IQNA

Ni nchi zipi zimeitangaza Jumapili kuwa Idul Fitr?

5:54 - March 30, 2025
Habari ID: 3480469
IQNA – Nchi kadhaa ulimwenguni kote zimethibitisha rasmi kuwa Jumapili, Machi 30, 2025, itakuwa siku ya kwanza ya Idul Fitr.

Katika eneo la Ghuba ya Uajemi_, Saudi Arabia imetangaza Idul Fitr kuwa Jumapili kufuatia 'kuthibitishwa' kuonekana kwa mwezi mwandamo wa Shawwal katika Kituo cha Astronomia  cha Tamir. Vivyo hivyo, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, na Kuwait pia zimethibitisha kuwa Idi itasherehekewa Jumapili baada ya kuthibitisha kuonekana kwa mwezi.

Palestina, na Yemen zimefanya zimetoa tamko sawa na hilo. Mufti wa al-Quds na Maeneo ya Wapalestina amethibitisha kuonekana kwa mwezi mwandamo, na kuthibitisha Jumapili kuwa siku ya kwanza ya Idi huko Palestina.  Huko Lebanon baadhi ya taasisi za Kiislamu zimetangaza Jumapili na zingine zimetangaza Jumatatu kuwa siku ya kwanza ya Idul Fitr kwa kutegemea Madhehebu.

Aidha, Uturuki imetangaza kuwa itasherehekea Idul Jumapili, ikitegemea mahesabu ya Kiastronomia na uthibitisho wa kuonekana kwa mwezi.

Wakati huo huo, nchi zingine zikiwemo Iran, Pakistan, Indonesia, Malaysia, Oman, Iraq, India, Syria, Brunei, Australia, Bangladesh, Morocco, Libya, Tunisia, Nigeria, Tanzania na Kenya zimethibitisha rasmi kuwa Jumapili itakuwa siku ya mwisho ya  Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Mataifa haya yataadhimisha Idul Fitr kuanzia Jumatatu, Machi 31.

Idul Fitr ni sikukuu kubwa ya kidini inayosherehekewa na Waislamu duniani kote, yenye Swala ya Jamaa,  sherehe, na utoaji wa msaada kwa wasiojiweza katika jamii ambao ni maarufu kama  Zakatul Fitri.

3492530

Kishikizo: idul fitr saudi arabia
captcha