Kwa mujibu wa taarifa, Sheikh Al-Azhar amejionea dharih (sehemu ya kuzikwa) mpya ya Msikiti wa Imam Hussein (AS) na maeneo mengine ya ndani na nje ya msikiti huo pamoja na ustawi jumla wa Haram hiyo takatifu.
Rais Abdel Fattah al-Sisi hivi karibuni alizindua Msikiti wa Imam Hussein (AS) mjini Cairo muda mfupi baada ya ukarabati wake kukamilika.
Katika uzinduzi huo, rais wa Misri hivi karibuni alitangaza juhudi za serikali ya Misri za kujenga upya maziara na maeneo yote yanayohusiana na Ahlul Bayt (AS) mjini Cairo na maeneo mengine ya Misri.
Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Misri imeanza mpango mkubwa wa ukarabati wa maeneo matakatifu na misikiti yenye mafungamano na Ahul Baty au watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad SAW.
Msikiti wa Imam Hussein (AS) ndio mkubwa zaidi kati ya misikiti ya Ahul Bayt AS, na ulijengwa karne ya sita Hijria.
Kwa mujibu wa baadhi ya riwaya, msikiti huu ni kaburi la kichwa cha Imam Hussein (AS). Msikiti wa Imam Hussein (AS) ni miongoni mwa misikiti muhimu sana katika ulimwengu wa Kiislamu na nchini Misri, na ni kitovu cha qiraa ya Qur'ani Tukufu nchini humo.