IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Kiislamu Duniani /3

Ushujaa wa Imam Ali katika Maneno ya Sheikh Muhammad Sadiq Arjun

14:15 - November 02, 2022
Habari ID: 3476021
TEHRAN (IQNA) – Sheikh Muhammad Sadiq Arjun (1903-1981), alikuwa mwanazuoni wa Al-Azhar nchini Misri ambaye aliandika vitabu vingi katika nyuga mbali mbali za sayansi ya Kiislamu. Moja ya vitabu vyake kinaitwa “Kamanda wa Waumini Ali ibn Abi Twalib (AS); Khalifa Bora Ambaye ni Mfano wa Kuigwa”.

Katika kitabu hiki, anaarifisha hulka njema na Sira ya Imam Ali (AS) na nafasi yake katika kumsaidia Mtume Muhammad (SAW).

Anazungumzia utoto wa Imam Ali (AS), mgogoro na njaa wakati huo na matukio mengine muhimu katika kipindi hicho.

Sheikh Arjun pia anazungumzia matukio ya baada ya kufariki Mtume Muhammad (SAW) na vilevile yale ya miaka ya mwisho ya maisha ya Imam Ali (AS).

Moja ya masuala anayoangazia katika kitabu hicho ni ushujaa wa Imam Ali (AS), ikiwa ni pamoja na katika Vita vya Uhud. Anaandika kwamba nusu ya wale 70 waliouawa katika vita hivyo waliuawa kwa upanga wa Imam Ali (AS). “Katika Vita vya Uhud, Mwenyezi Mungu aliwajaribu Waislamu na wote waliokuwa karibu na Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) walitawanyika isipokuwa Ali (AS) ambaye alibaki karibu na Mtume (SAW) na alikuwa shujaa wa Uislamu.”

Ilikuwa hapa ambapo jukumu la Imam Ali (AS) lilibainika kwa sababu alikaa kando ya Mtume Muhammad (SAW) kwa ushujaa wa kipekee na akamlinda dhidi ya mashambulizi ya mara kwa mara ya makafiri.

Katika Vita vya Khandaq (Vita vya Handaki), Waislamu walipowekwa chini ya mzingiro, mtu mmoja aitwaye Amr ibn Abd Wudd kutoka upande wa adui aliwapinga Waislamu. Alikuwa mmoja wa mashujaa na watu mashujaa wa Uarabuni wakati huo wakati Ali (AS) akiwa kijana. Ali(AS) akaenda kupigana naye na akamshinda.

Ngome za Khaybar pia zilitekwa na Imam Ali (AS). Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) alimwambia Imam Ali (AS) katika Vita vya Khaybar: “Wallahi, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuongoza mtu mmoja (katika Uislamu) kupitia kwako, ni bora kwako kuliko ngamia wa thamani zaidi.”

Imam Ali (AS) hakushiriki katika vita moja tu na hivyo vilikuwa ni Vita vya Tabouk na hiyo ilikuwa ni kwa sababu Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) alimuamuru abaki Madina. Haya yametajwa katika Hadithi ya Al-Manzilah ambamo Mtume (SAW) alimwambia Imam Ali (AS): "Wewe kwangu mimi ni wa hadhi ya Harun kwa Musa, isipokuwa hakuna Mtume baada yangu."

Mtukufu Mtume (SAW) alipohama kutoka Makka kwenda Madina katika usiku wa Hijra, alimpa jukumu binamu yake Imam Ali (AS) kulala juu ya kitanda chake na kuvaa nguo za Mtume (SAW) ili makafiri wasitambue kutokuwepo kwake.

Moyo wa kijana Ali (AS) ulijawa na roho ya uaminifu na ushujaa. Alilala juu ya kitanda cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika nyakati za hatari sana na alikuwa tayari daima kujitolea maisha yake kwa ajili ya Mtume (SAW).

Aliunga mkono bendera ya Jihad iliyokuwa mikononi mwa Mtume (SAW), alipigana na maadui katika vita mbalimbali bila kujali idadi ya Waislamu ilionekana kuwa ndogo kwa kulinganisha na ya adui, na akageuza khofu katika nyoyo za Waislamu. amani, utulivu na usalama.

Kishikizo: imam ali as Arjun
captcha