IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu/6

Saher Al-Kabi; Maonyesho ya uzalendo huko Palestina kwa kaligrafia

12:31 - December 15, 2022
Habari ID: 3476251
TEHRAN (IQNA) – Ili kupambana dhidi ya wavamizi au kuimba kauli mbiu za kizalendo, mwanaharakati haishii kwenye shughuli za kisiasa au mapambano ya silaha. Wasanii wanafanikisha mapambano yao bila kuingia kwenye ulimwengu wa siasa.

Mmoja wa wasanii kama hao ni mwandishi wa kaligrafia wa Kipalestina Saher al-Kabi ambaye huwasilisha hisia zake za uzalendo kwa kazi zake nzuri za uandishi.

Kazi za msanii wa Kipalestina zinaonyesha harakati zake za mara kwa mara zilizowasilishwa maandishi ya Kiarabu nna daima yuko katika harakati ya kuimarisha ujuzi na ubunifu wake.

Kazi zake haziwezi kuainishwa katika mfumo wa sanaa za jadi na za kuiga. Daima anajaribu kuunda kazi mpya  katika kaligrafia ya Kiarabu.

Saher anatumia zana mbalimbali za sanaa na mbinu za calligraphy na ametiwa msukumo na maandishi ya kidini na matakatifu, utamaduni na fasihi ya Kiarabu na urithi wa simulizi wa Palestina. Kazi zake ni pamoja na uandishi wa maandishi ya aya za Qur'ani Tukufu, Hadith za Mtukufu Mtume Muhammad (SAW), na ushairi wa Kiarabu na Kipalestina.

Katika moja ya kazi zake, ameandika beti za kaligrafia za shairi maarufu la Imam al-Shafi’i. Mtindo anaotumia ni mtindo wa unaojulikana kama Muraqqa.

Miongoni mwa kazi zake nyingine ni kaligrafia ya mashairi yaliyoandikwa na mshairi wa Imarati Saqr bin Sultan Al Qasimi akiwasifu Wapalestina na Palestina.

Katika sanaa yake ya kaligrafia, Saher pia anatumia alama za kitaifa za Palestina. Mara nyingi ameandika mashairi ya mshairi wa Kipalestina Mahmoud Darwish yenye mada kama vile uzalendo, utambulisho, lugha, ardhi na nchi.

Katika mojawapo ya kazi zake kuhusu Palestina, amezingatia kadhia ya nchi ya asili ili kukkuza uelewa wa msomaji kuhusu utaifa

Rangi pia ina nafasi muhimu katika kazi zake. Kwa mfano katika shairi la Mahmoud Darwish, ameandika neno ardhi kwa kalligrafu kwa wino mweusi na maneno mengine kwa wino mwekundu.

captcha