IQNA

Haram ya Imam Ali (AS) yapambwa kwa maua katika maadhimisho ya kuzaliwa kwa Bibi Zahra (AS)

16:56 - December 10, 2025
Habari ID: 3481640
IQNA – Kadiri siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bibi Fatima Zahra (AS) inavyokaribia, maelfu ya matawi ya maua halisi yamepamba uwanja na ukumbi wa haram tukufu ya Imam Ali (AS).

Kitengo cha Mapambo kimeendelea na kazi zake za maandalizi ya kusherehekea tukio hili lenye baraka. Katika siku za karibuni, kitengo hicho kimekuwa kikihusika na mapambo na mpangilio wa maua katika haram ya Amirul-Mu’minin (AS) na baraza zake tukufu.

Baraq Hadi, mkuu wa Kitengo cha Mapambo, aliueleza kituo cha habari kuwa maandalizi ya mwaka huu yamejumuisha kuweka shada za waridi halisi katika korido na baraza za haram tukufu, ambapo zaidi ya matawi 11,000 ya waridi yametumika.

Aliongeza kuwa kitengo hicho pia kimekamilisha mapambo ya korido za uwanja wa Bibi Fatima (AS) pamoja na maandalizi ya sherehe maalumu za Wiki ya Ifaf (Wiki ya Staha), na shughuli zake mbalimbali ndani ya haram, zenye lengo la kuonyesha uzuri na utukufu wa tukio hili.

Sheikh Hadi alifafanua kuwa kazi hizi ni sehemu ya mpango mpana uliotayarishwa na Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Ali (AS kwa ajili ya kuadhimisha tukio hili lenye baraka, kuunda mazingira ya kiroho yanayostahiki hadhi ya Bibi Zahra (AS), na kuimarisha thamani ya ifaf (usafi wa moyo na mwili) katika mji mtukufu wa Najaf.

Tarehe 20 ya mwezi wa Jumada al-Thani katika kalenda ya Hijria, ambayo mwaka huu inalingana na Alhamisi, Desemba 11, ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa binti mpenzi wa Mtume Mtukufu Muhammad (SAW). Tukio hili pia huadhimishwa kama Siku ya Mwanamke na Siku ya Mama.

3495689

Habari zinazohusiana
captcha