IQNA

Ustawi wa Iran

Makombora mapya ya Iran ya Bavar 373 na Sayyad B4

18:37 - November 06, 2022
Habari ID: 3476044
TEHRAN (IQNA)- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua mfumo mpya wa makombora ya kujihami ya masafa marefu ya Bavar (Kujiamini) 373 na pia imefanyia majaribio kombora jipya la Sayyyad B4 leo Jumapili.

Mfumo wa Bavar-373 wa makombora ya kijihami yenye uwezo wa kuruka umbali wa kilomita 300 umezinduliwa sambamba na kuanza uundwaji kwa wingi makombora ya Sayyad B4.  Uzinduzi wa mafanikio hayo ya kijeshi umefanyika katika sherehe iliyohudhuriwa na Waziri wa Ulinzi Brigadier-General Mohammad-Reza Ashtiani.

"Mfumo wa Bavar-373 awali ulikuwa na uwezo wa kulenga shabaha umbali wa kilomita 200 na sasa umeimarishwa na unaweza kulenga ndege za kivita zilizo umbali wa kilimota 300," amesema Waziri wa Ulinzi. Amesema mfumo mmoja unaweza kulenga maeneo sita kwa wakati mmoja kutokana na teknolojia ya hali ya juu iliyotumika.

Uzalishaji wa mfumo wa makombora wa Sayyad B4 pia umezinduliwa leo na hivyo kuongeza idadi ya makombora ya kujihami ya Iran. 

Hayo yanajiri wakati ambao jana Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) lilizindua kwa mafanikio roketi la kubebea satalaiti la Qaem-100 katika anga za mbali.

Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh, Kamanda wa kikosi cha anga za mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na maafisa wengine wa ngazi za juu wa Majeshi ya Iran wameshiriki katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika jana Jumamosi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh amesema madola ya kibeberu yakiongozwa na Marekani yanafanya kila yawezalo ili kuzuia ustawi wa Iran, kwa kuwa yanashindwa kustahamili mafanikio ya kustaajabisha ya Jamhuri ya Kiislamu.

Roketi la kubebea satalaiti la Qaem-100 lina uwezo wa kuweka satalaiti zenye uzani wa hadi kilo 80 katika anga za mbali, umbali wa kilomita 500 kutoka ardhini.

Roketi la kubebea satalaiti la Qaem-100 lina uwezo wa kuweka satalaiti zenye uzani wa hadi kilo 80 katika anga za mbali, umbali wa kilomita 500 kutoka ardhini.

Kamanda huyo wa kikosi cha anga za mbali cha Jeshi la IRGC ameeleza bayana kuwa, "Vijana wa Iran wamevishinda vikwazo shadidi zaidi katika historia, na kupata mafanikio kama haya."

موشک صیاد ۴B رونمایی شد + عکس

موشک صیاد ۴B رونمایی شد + عکس

موشک صیاد ۴B رونمایی شد + عکس

4097319

captcha