IQNA

Rais Hassan Rouhani

Uwezo wa majeshi ya Iran ni kwa ajili ya kujihami na kutoa jibu litakalomfanya adui ajute

19:45 - June 14, 2021
Habari ID: 3474005
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uwezo wa vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ni kwa ajili ya kujihami na kutoa jibu litakalomfanya adui ajutie.

Rais Rouhani ambaye mapema leo alikuwa akihutubia katika uzinduzi wa miradi kadhaa ya kitaifa ya Wizara ya Ulinzi, ameongeza kuwa, Iran sasa ni nguvu kubwa inayodhamini usalama wa nchi jirani.

Amesema kuwa, katika kipindi cha vita vya kulazimishwa vya miaka 8 uwezo wa Jeshi la Anga la Iran umeimarika zaidi kuliko kipindi kingine chochote.
Rais Rouhani amesema, katika kipindi hicho Iran imefanikiwa kutengeneza zana za kisasa za anga na kuzidisha uwezo wake wa kimakombora. Vilevile imefanikiwa kutengeneza manowari za kivita, nyambizi na makombora yanayohitajiwa na kikosi cha wanamaji. Amesema Iran imefanikiwa kuzidisha masafa ya kombora la majini la Cruise kutoka kilomika 300 hadi elfu moja.

Vilevile ameashiria uwezo wa Iran katika masuala ya anga kama uundaji wa ndege ya kivita ya Kauthar, injini za ndege na kadhalika na kusema: Hii leo jeshi la Jamhuri ya Kiislamu na vikosi vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) vimefikia kiwango cha kujitosheleza na kujitegemea. 

Amesisitiza kuwa, uwezo wa jeshi la Iran ni kwa ajili ya kujihami na kwamba kamwe serikali ya Iran haijawahi na haina nia ya kuivamia au kuishambulia nchi yoyote.   

Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo limepokea meli mbili mpya za kivita ambazo zimeundwa kikamilifu hapa nchini.

Manoari mbili ambazo ni meli ya kisasa ya kivita iliyopewa jina la Dena na meli ya kuondoa mabomu yaliyotegwa baharini iliyopewa jina la Shahin zimezinduliwa leo katika mji wa pwani wa Bandar Abbas kusini mwa Iran.

3977393

Kishikizo: iran ، rouhani ، rais rouhani ، Majeshi
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha