IQNA

Nukuu kutoka Nahjul-Balagha / 2

Mtazamo wa Imam Ali kuhusu Tauhidi

16:12 - November 15, 2022
Habari ID: 3476092
TEHRAN (IQNA) – Imam Ali (AS) anaashiria kwenye vipengele vya tauhidi safi katika Khutba ya 1 ya Nahj al-Balagha.

Nahjul Balagha ni mkusanyiko wa khutba, barua na maelekezo ya Imam Ali (AS). Mengi yamesemwa kuhusu ubora na ufasaha wa maneno yaliyomo katika khutba na barua hizo. Kwa ufupi, Nahj al-Balagha ni kilele cha ufasaha.

Katika mfululizo wa vikao, Emad Afroogh anajaribu kutambulisha mawazo ya Imam Ali (AS). Huu hapa ni muhtasari wa kikao cha pili:

Katika kikao hiki, niliamua kurejea Khutbah (mahubiri) ya kwanza ya Nahjul Balagha.

Hapa, Imam Ali (AS) anazungumzia mojawapo ya sentensi bora kuhusu tauhidi. Anasema: “La kwanza katika dini ni kumtambua yeye, na ukamilifu wa kumtambua ni kumsadiki, na ukamilifu wa

kumsadiki ni kumpwekesha. Na ukamilifu wa kumpwekesha ni kumtakasa na ukamilifu wa kumtakasa ni kumuepusha mbali na sifa. Na mwenye kumsifu Mwenyezi Mungu. Atakuwa amemuambatanisha, na mwenye kumuambatanisha amemfanya kuwa wawili, na mwenye kumfanya kuwa wawili atakuwa amemfanya kuwa mwenye sehemu sehemu, na mwenye kumfanya kuwa mwenye sehemu sehemu atakuwa hamjui Mwenyezi Mungu , na asiyemjua atakuwa amemuonyesha, na mwenye kumuonyesha atakuwa amemwekea mipaka, na mwenye kumuwekea mipaka atakuwa amemuhisabu. Na mwenye kusema yuko ndani ya nini? Anakuwa amemwingiza Mwenyezi Mungu ndani ya kitu.

Kutafakari kwa kina juu ya khutba hii, mtu anaweza kuona vipengele tofauti vya Tawhid na matokeo yake kufikia tauhidi safi.

Zaidi ya hayo, sehemu nyingine ya khutba hii inatoa msaada mkubwa kwa wale wanaofahamu theolojia.

Na mwenye kusema yuko juu ya nini? Atakuwa amemtoa humo. Amekuwa yupo sio kwa kutukia, yupo lakini sio kwa maana ya hakuwapo hapo kabla. Yuko pamoja na kila kitu si kwa mwambatano wa kimwili. Yutafauti na kila kitu si utafauti wa kimwili, mtendaji sio kwa maana ya harakati za kimwili na vyombo, mwenye kuona pindi hakuna wakuonwa kati ya viumbe wake. Yu pweke pindi hakuna mkazi analiwazika naye wala haoni ukiwa kwa kukosekana kwake.

Profesa Richard Swinburne, mwanafalsafa Mkristo mashuhuri, pia anaamini katika dhana kama hiyo anaposema kwamba Mwenyezi Mungu hana mwili wa kimwili kwa sababu kama angekuwa nao, angekabili mipaka. Kwa sababu hii, anaweza kuwepo katika maeneo mbalimbali wakati moja.

Kishikizo: tauhidi imam ali as
captcha