IQNA

Nukuu kutoka kwa Nahj al-Balagha /3

Utawala wa misingi ya Mwenyezi Mungu; Njia ya Kufikia Malengo ya Juu

16:49 - December 03, 2022
Habari ID: 3476189
TEHRAN (IQNA) – Kwa mtazamo wa Imam Ali (AS), serikali ni njia tu ya kufikia malengo ya juu kama vile uadilifu wa kijamii. Mtazamo huu unaonekana kwa uzuri katika kitabu kikuu Nahj al-Balagha, ambacho ni mkusanyo wa maneno yake.

Haya ni kwa mujibu wa Emad Afroogh, mwanasosholojia na mtafiti wa masuala ya kidini akizungumza katika mfululizo wa vikao vya kutambulisha fikra za Imam Ali (AS). Huu hapa ni muhtasari wa kikao cha tatu:

Khutba ya tatu ya Nahj al-Balagha inakosoa hali za wakati huo na hatua ya baadhi ya watu kuchukua hatua dhidi ya yale aliyoyataka Mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Bila shaka inawezekana kwamba Khutba hii imehusiana na suala la Ukhalifa (urithi) wa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Lakini bila kujali hilo, Khutba inapaswa kuangaliwa kwa jinsi Imam Ali (AS) anavyouona utawala.

Katika sehemu ya Khutba, Imam (AS) anasema: “... Nilijikinga nao kwa nguo na nikajiweka kando nao. Nikajifikiria, je! Nishambulie na mkono butu, au nilivumilie giza la upofu, mtu mkubwa humo huzeeka, na mdogo humo huwa kijana, muumini anataabika humo mpaka akutane na Mola wake, nikaona kuivumilia hali hii ni busara, basi nikasubiri hali jichoni mwangu muna utongotongo, na kooni kuna kitu kilichokwama. Naiona mirathi yangu imepokonywa…"

Maneno haya ya Khutba hizi yanapaswa kuwa somo kwa kila serikali inayotaka kufuata nyayo za serikali ya Imam Ali (AS).

Katika sehemu nyingine ya Khutba hii, Imam Ali (AS) anasema: “(Kwa hakika wameshirikiana viwele vyake viwili wao kwa wao tu, huyu mmoja ameuweka (ukhalifa) katika upande ulio mgumu, mguso wake wakwaruza, kujikwaa kunakithiri na kuomba udhuru, aliyekuwa nao ni kama aliyepanda ngamia machachari asiyepandika: akimvuta hatamu atamkaba na akimlegezea atamtupa kweye maangamizi, hapo wallahi watu watapatwa na myumbo, uovu na kupotoka, Nilivumilia kwa muda mrefu wote huo, ingawaje ulikuwa mtihani mgumu.”

Katika sehemu tofauti za Nahj al-Balagha, Imam (AS) anawaonya watawala kutowalazimisha wanyonge kufanya mambo kinyume na matakwa yao wala kutumia mabavu na vitisho dhidi yao. Mtawala anapaswa kufuatilia na kudhibiti tu mambo katika jamii.

Amirul-Muuminina anautazama utawala kuwa ni njia ya kufikia mwisho na mwisho huo sio kutojali njaa ya wanyonge huku madhalimu wanajilimbikizia mali.

Imam Ali (AS) anasema kwa uwazi kwamba kama Mwenyezi Mungu hajaweka ahadi naye na na wanachuoni kutojali masuala haya, angeacha kuwa Khalifa.

Kutoka kwenye Khutba ya tatu ya Nahj al-Balagha mtu anaweza kupata nadharia ya uhalali, uhalali ambao ni mchanganyiko wa vipengele viwili: uhalali na kukubalika (umaarufu).

Imam Ali (AS) ana haki na uhalali wa kidini lakini kabla ya watu kuja kwake na kuweka kiapo cha utii kwake, kipengele cha uhalali kilikuwa hakijatekelezwa. Kwa hiyo uhalali una vipengele viwili: haki na kukubalika (na watu).

Kishikizo: nahjul balagha ، imam ali as
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha