IQNA

Nukuu kutoka kwa Nahj al-Balagha / 1

Mwelekeo wa itikadi ya Mungu Mmoja katika Mawazo ya Imam Ali

16:07 - November 15, 2022
Habari ID: 3476091
TEHRAN (IQNA) – Mwanasosholojia na mtafiti anasema tunapaswa kuwa na ufahamu mpya wa Imam Ali (AS) kwani alikuwa mwanafikra wa hadhi ya juu na hilo linadhihirika wakati unaporejea kwenye vipengele vya kimaanawi na kiroho vya fikra zake.

Fikra za Imam Ali AS zinapatikana katika kitabu kinachojulikana kama Nahjul Balagha. Kitabu hiki ni mkusanyiko wa khutba, barua na maelekezo ya Imam Ali (AS). Mengi yamesemwa kuhusu ubora na ufasaha wa maneno yaliyomo katika khutba na barua hizo. Kwa ufupi, Nahj al-Balagha ni kilele cha ufasaha.

Katika mfululizo wa vikao, Profesa Emad Afroogh anajaribu kutambulisha mawazo ya Imam Ali (AS). Huu hapa ni muhtasari wa kikao cha kwanza:

Miongoni mwa vitabu ambavyo nimevisoma, viwili kati ya hivyo vinanivutia; The City of God and Confessions kilichoandikwa na na Augustine wa Hippo. Baada ya hapo, nilihisi hamu ya kuipitia Nahj al-Balagha.

Mahusiano kati ya vitabu hivi ni muhimu. Augustine na Imam Ali (AS) wana sehemu maalum miongoni mwa Wakristo na Waislamu mtawalia na wote wawili wanazungumzia kukiri. Dhana ambazo Imam Ali (AS) anaziweka mbele katika dua ya Kumayl zinaelekeza kwenye aina ya ungamo. Ingawa, kunaweza kuwa na tafsiri tofauti za hiyo.

 “Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe dhambi zangu zinazo vunja ulinzi! Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe dhambi zinazo teremsha maovu! Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe dhambi zinazozuia dua!” inasoma sehemu ya dua na hili si somo la jinsi ya kuomba. Kinachoelezwa kuwa ni amali njema kwa watu wema kweli kinaweza kuwa ni dhambi kwa wale walio na vyeo vya juu na wako karibu zaidi na Mwenyezi Mungu. Bila hisia ya kuwa mtenda dhambi, Imam Ali (AS) asingeweza kufikia nafasi hiyo ya juu. Kuna baadhi ya nukta zinazohitaji kuelezwa kuhusu sifa ya Imam Ali (AS).

Ninaamini kwamba Imam Ali (AS) alikuwa msikivu kwa matatizo na dhulma na hakuweza kupuuza masuala ya watu.

Leo, kwa bahati mbaya tunashuhudia kwamba wale wahusika wasiojali maumivu yaw engine ndio ambapo wanapata sifa za juu na kupandishwa vyeo. Ikiwa mtu ana huzuni na hasira na ukandamizaji, tabia yake itaulizwa.

Tunapaswa kufanya uchunguzi wa  kina kumhusu Imam Ali (AS) na kazi ambazo zinanasibishwa naye. Kumuona Imam Ali (AS) pekee kama mtu mtakatifu kutatuzuia sisi kuelewa mawazo na utambuzi wake wa juu.

Imam Ali (AS) ni mtakatifu kwa sababu mawazo yake ni makubwa na ya kiungu. Utakatifu wake unarudi kwenye mwelekeo wa kiroho na wa kiungu wa mawazo yake. Tukimsoma, tutaelewa ukuu wa tabia yake.

Ewe Ali! Uchungu ni kwamba wamekusahau wewe si mtu wa maneno bali ni mtu wa utekelezaji! Hukukubali serikali ili watu wasikie maneno mazuri, bali ulikuja ili watu washuhudie matendo mema na ya haki. Ewe Ali! Vitabu na mashairi yanaandikwa ili kukusifu lakini hakuna mtu anayetafuta mafundisho yako kwa vitendo; ukweli wa kutafuta uhuru, kutafuta haki, usambazaji wa haki wa Bayt al-mal, na ukweli wa maadili na kiroho.

captcha