Utafiti wa vyuo vikuu vya Lucerne na Friborg nchini Uswizi unasema ujuzi kuhusu Uislamu unaweza kuzuia itikadi kali. "Shule ni sehemu isiyoegemea upande wowote," anasema mkurugenzi wa utafiti huo Hansjörg Schmid. Hii ina maana pia kwamba watoto kutoka asili tofauti za Kiislamu hupokea masomo pamoja.
Kwa kuongezea, mkazo zaidi unawekwa kwenye mitaala ya masomo yake shuleni. "Walimu wa Kiislamu wanalazimika kuwasilisha dhana zao shuleni," anasema Schmid. "Hii inafanya udhibiti wa ubora iwezekanavyo."
Mkurugenzi wa Kituo cha Uislamu na Jamii cha Uswizi katika Chuo Kikuu cha Fribourg, pamoja na watafiti wengine watatu, wamechunguza mafundisho yote ya Kiislamu yanayotolewa shuleni.