IQNA

Mmarekani amdunga kisu na kumuua mtoto wa Kipalestina

9:46 - October 17, 2023
Habari ID: 3477744
WASHINGTON, DC (IQNA) – Mzungu mwenye umri wa miaka 71 katika jimbo la Illinois nchini Marekani aliyechochewa na chuki dhidi ya Waislamu na Wapalestina, amemuua kwa kumdunga kisu mara 26 mtoto wa Kiislamu mwenye umri wa miaka 6 na kumjeruhi vibaya mama yake.

Tukio hilo lilijirii jana Jumapili huku wanasiasa wa Marekani na vyombo vya habari vikiendelea kufanya uchochezi dhidi ya Waislamu kufuatia vita vya Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa na Wazayuni.

Polisi wa Marekani wanasema Joseph Czuba, (71) wa Illinois alimdunga kisu moyoni na kwenye shingo mtoto huyo wa Kiislamu, Wadea Al-Fayoume, huku akimjeruhi vibaya mama yake. Ripoti zinasema Czuba alikuwa akitoa nara na kauli za kupiga vita Uislamu na Wapalestina wakati anatekeleza ukatili huo. "Mnapaswa kufa, nyinyi Waislamu", amesema Mmarekani huyo huku akimdunga kisu mtoto huyo wa Kipalestina

Mama yake Wadea Al-Fayoume, mwenye umri wa miaka 32 pia alidungwa kisu mara nyingi katika shambulizi lililotokea kwenye kitongoji cha Plainfield, takriban maili 40 (kilomita 64) kusini magharibi mwa Chicago.

Polisi ya Marekani imemtuhumu Joseph Czuba kwa kufanya uhalifu uliochochewa na chuki na kusisitiza kuwa wahanga hao wawili walilengwa kwa sababu ya imani yao ya Kiislamu, katika muktadha wa vita ambayo Israel inaendeleza dhidi ya Wapalestina.

Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR) pia limelaumu matamshi ya chuki yanayoenezwa kwa wingi na wanasiasa na vyombo vya habari nchini humo dhidi ya Uislamu.

Taarifa iliyotolewa na CAIR kwenye mtandao wa kijamii wa X  imesema: "Tumeshtushwa na kufadhaishwa kujua kwamba mwenye nyumba huko Chicago amedhirisha chuki yake dhidi ya Uislamu na Wapalestina akivamia nyumba ya familia ya Waislamu, kuwashambulia kwa kisu na kumjeruhi mama na kumuua mtoto wake mwenye umri wa miaka 6, Wadea Al. -Fayoume.

 

3485596

captcha