Mahmoud Abdulhakam; Qari wa Misri mwenye sauti Iliyojaa unyenyekevu
IQNA – Sheikh Mahmoud Abdulhakam alikuwa miongoni mwa maqari wakubwa wa Misri ambaye alikuwa na mtindo wake maalum wa usomaji Qur’ani Tukufu na hakuwaiga wasomaji wengine.
Ijumaa Septemba 13, iliadhimisha kumbukumbu ya miaka 42 ya kifo cha Sheikh Abdulhakam ambaye pia alikuwa miongoni mwa wanachama waanzilishi wa Jumuiya ya Wasomaji Qur'ani wa Misri.
Abdulhakam alizaliwa mnamo Februari 1, 1915 katika Kijiji kimoja cha Jimbo la Qena nchini Misri.
Alianza kujifunza Qur’ani katika umri mdogo katika Maktab (shule ya jadi ya Qur'ani) ya kijiji hicho.
Baba yake kisha akampeleka katika Taasisi ya Qur'ani ya Ahmadi huko Tanta ambako alijifunza Tajweed na usomaji Qur’ani kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar.
Punde si punde akawa qari mashuhuri nchini Misri pamoja na nchi nyingine za Kiarabu na Kiislamu.
Mnamo mwaka wa 1940, yeye, pamoja na maqari wengine maarufu kama Sheikh Mohamed Rif'at, Sheikh Ali Mahmoud na Sheikh al-Saifi, walianzisha Jumuiya ya Wasomaji Qur'ani wa Misri na akawa mweka hazina wake wa kwanza.
Alikuwa mfano wa kuigwa katika suala la juhudi zake za kutumikia na kukuza usomaji wa Qur'an Tukufu nchini Misri na maeneo mengine duniani/
Alishiriki katika vikao vya usomaji Qur’an huko Misri na nchi zingine kwa zaidi ya miaka 37 hadi kifo chake.
Abdulhakam alikuwa na sauti nzuri iliyojaa unyenyekevu, sauti iliyogusa mioyo ya wasikilizaji.
Pia alijitolea kusahihisha usomaji na kuwa na mtindo wake mwenyewe badala ya kuwaiga maqari wengine.
Alikuwa mchamungu na alikuwa na shauku kubwa ya kuitumikia Qur’ani na kueneza sanaa ya usomaji wa Qur'ani kote ulimwenguni.
Alikuwa na watoto wanane, ambapo binti zake wawili waliolewa na watoto wawili wa kiume wa qari mwingine mashuhuri, Sheikh Mohamed Sidiq Minshawi.
Sheikh Mahmoud Abdulhakam aliaga dunia na kurekea kwa Mola wake Septemba 13, 1982.
Hapa chini ni mojawapo ya visomo vyake vya Qur’ani.
3489899