Kiongozi Muadhamu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema, alikubali siku ya Jumatano kutoa msamaha au kupunguza adhabu za wafungwa wa Iran kufuatia pendekezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mahakama, Hujat-Al-Islam Gholam Hossein Mohseni Ejei, ambaye aliomba msamaha wa Kiongozi kwa wafungwa waliotimiza masharti maalum.
Jumla ya wafungwa 3,126 walipata msamaha huo.
Katika barua yake, Hojat-ol-Islam Mohseni Ejei aliomba msamaha huo kwa mnasaba wa siku tukufu za Eid al-Mab’ath, Idi za mwezi wa Shaaban katika kalenda ya Hijria, na kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Kifungu cha 110 cha Katiba kinampa Kiongozi mamlaka ya kutoa msamaha au kupunguza adhabu za wafungwa kwa mapendekezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mahakama.
Mapinduzi ya Kiislamu Yalivunja Ushawishi wa Madikteta: Mkuu wa Mahakama ya Iran
Hata hivyo, msamaha huu hauwahusu wafungwa wa makosa fulani, ikiwa ni pamoja na wale waliopatikana na hatia ya:
Usafirishaji haramu wa dawa za kulevya kwa kutumia silaha
Biashara haramu ya silaha
Utekaji nyara
Mashambulizi ya tindikali
Ubakaji
Uporaji wa kutumia silaha
Rushwa
Ubadhirifu wa mali ya umma
Utengenezaji wa fedha bandia
Utakatishaji fedha
Uvurugaji wa uchumi
Usafirishaji wa pombe
Magendo ya bidhaa kwa mtandao wa uhalifu uliopangwa.