Mmoja wa wanachama wa msafara huo wa Qur’ani alisoma Qur’ani Tukufu ndani ya Mawkib moja huko Karbala.
Mawkib ni vituo vya huduma vilivyo katika maeneo ya kidini ya Waislamu wa madhehebu ya Shia au wakati wa matukio ya kidini ya Mashia ambapo wafanyaziara na watu wengine wote katika eneo husika wanaweza kupokea chakula, chai, na sharbat (vinywaji vitamu) n.k na pia kupata sehemu ya kupumzika.
Wanachama wa ujumbe huu walifanya programu mbalimbali za Qur’ani kwa ajili ya wafanyaziyara wa Arbaeen wakati wa ukaaji wao nchini Iraq.
Mehdi Gholamnejad na Mehdi Taghipour, maqari wawili maarufu kutoka Iran, walikuwa katika msafara huo na wakasoma aya tukufu wakati wa matembezi ya kuelekea kwenye haram mbili tukufu mjini Karbala.
Ifuatayo ni qira’a yao ya Qur’an Tukufu ndani ya Mawkib ya Atabat Muqaddasayn katika mji mtukufu wa Karbala:
4299990