IQNA

Arbaeen katika Qur'an /3

Arbaeen ni nambari inayohusiana na ukuaji wa ubora wa Mwanadamu

15:21 - August 19, 2024
Habari ID: 3479302
IQNA – Wakati Arbaeen, maana yake ni arobaini na arubaini, ni neno linalohusiana na wingi, katika maandiko mengi ya Kiislamu na Hadithi, linatumika kurejelea sifa na ukuaji wa kiroho wa mwanadamu.

Arbaeen ni nambari ya kimaanawi ambayo matumizi yake katika aya za Qur'ani Tukufu na Hadithi yanaonyesha kuna siri nyingi zilizofichwa ndani yake.

Manabii wa Mwenyezi Mungu na waja wema au mawalii wa Mwenyezi Mungu daima wameheshimu Arbaeen na kuacha urithi mkubwaunaohusiana na dhana ya Arbaeen.

Kwa hakika, neno Arbaeen, ambalo linahusiana na kiasi, linatumika kurejelea sifa katika sayansi ya Irfani ya Kiislamu ambapo Hadithi kuhusu Arbaeen mara nyingi huvuta fikira kwenye ukuaji wa kiroho.

Mitume wengi wa Mwenyezi Mungu, akiwemo Mtume Muhammad (SAW), waliteuliwa utume wakiwa na umri wa miaka 40. Labda sababu ni kwa sababu mtu anaweza kuanza ukuaji wa kiroho akiwa na umri wa miaka 40, lakini inakuwa vigumu baada ya hapo.

Matumizi ya nne ya Arbaeen katika Quran (nyingine tatu zilizotajwa katika makala zilizotangulia) ni katika Surah Al-Ahqaf na inahusu ardhi ya ukuaji wa mwanadamu:

" Na tumemuusia mwanaadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini. Hata anapo fika utu uzima wake, na akafikilia miaka arubaini, husema: Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayo yapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu.” (Aya ya 15 ya Surah Al-Ahqaf).

Msemo “...Hata anapo fika utu uzima wake, na akafikilia miaka arubaini...” unaonyesha kwamba zama hizi ni zama za ukamilifu wa akili na uwezo wa juu kabisa wa ukuaji.

Kwa mujibu wa Hadith ya kinabii, mtu anayejitoa kwa dhati kwa Mungu kwa muda wa siku arubaini, mito ya hekima itatiririka kutoka moyoni mwake hadi kwenye ulimi wake.

Kwa maneno mengine, kutakasa matendo ya mtu kwa Mungu kwa siku 40 kutaathiri moyo wake na kumsaidia kutambua mafundisho kwa kina

3489534

Kishikizo: arbaeen qurani tukufu
captcha