"Ni muhimu kuimarisha mkusanyiko muhimu wa Arbaeen ili kupanua na kukuza utamaduni wa Qur'ani," Hujjatul Islam Ali Taghizadeh, Mkuu wa Shirika la Dar-ul-Quran la Iran, alisema katika mazungumzo na IQNA Jumanne.
Maadhimisho ya Arbaeen hufanyika siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye aliuawa shahdii na jeshi la Yazid katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa na 680 Miladia.
Kila mwaka mamilioni ya Mashia na pia idadi ya wasiokuwa Mashia humiminika Karbala, mji ulipo Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) kufanya ibada za maombolezo. Wafanya ziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri mamia ya kilomita kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Karbala.
Arbaeen ya mwaka huu inatarajiwa kuanguka mnamo Agosti 25, kulingana na kuonekana kwa mwezi.
Sheikh Taghizadeh alibainisha kwamba wakati wa Arbaeen na matukio mengine yanayohusiana na Ahl al-Bayt (AS), lengo kuu ni kujikurubisha na Qur’ani Tukufu, Mtume Muhammad (SAW) na kuwa na mapenzi ya dhati kwa Ahlul-Bayt (AS). "Tunapaswa kuelekeza upendo huu maarufu kwa Imam Hussein (AS) na Ahlul-Bayt (AS) kwenye kustawisha mapenzi kwa Qur'ani."
"Ni muhimu kuangazia ni kwa kiasi gani Imam Hussein (AS) na Ahl al-Bayt (AS) walivyoithamini Qur'ani Tukufu," alisisitiza.
/3489402