"Siku chache kabla ya kuanza safari ya Ziyara kwa miguu kutoka Mashhad hadi Karbala tuliamua kuandika aya za Qur'ani wakati wa safari yetu kuelekea kwenye Haram ya Imam Hussein (AS)," Mohammad Fatehi Peykani, mfanyakazi mstaafu wa benki, aliiambia IQNA.
"Katika muda wa siku sabini na mbili za kutembea, tulitumia vipindi vyetu vya mapumziko kuandika aya za Qur'ani Tukufu," aliongeza.
Aliungana na Khalil Taheri katika safari na mradi huu wa kiroho.
Anasema wamekamilisha kuandika nusu ya aya Qur'ani katika hati ya Nasta'liq hadi sasa.
"Mwishoni mwa kila ukurasa, tunaona mahali ambapo ukurasa huo mahususi wa Qur'ani uliandikwa, ambayo inasaidia kuhifadhi kumbukumbu za safari hii ya kiroho," Fatehi aliongeza.
Arbaeen ni tukio la kidini linaloadhimishwa na Waislamu, hasa wa madhehebu ya Shia, katika siku ya arobaini baada ya Siku ya Ashura, kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na imamu wa tatu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Ni miongoni mwa safari kubwa zaidi za kila mwaka duniani, huku mamilioni ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wakitembea kuelekea Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Mwaka huu, siku ya Arbaeen iliangukia tarehe 25 Agosti.
"Tunatumai kumaliza sehemu iliyobaki ya Qur'ani karibu na Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) na kisha kuwasilisha hati iliyofungwa kwenye wasimamizi wa eneo hilo takatifu," Fatehi alisema.
"Katika nakala hii, tuliamua kwamba baada ya kukamilisha kila ukurasa, tutaandika maelezo ya dhana na tafsiri kuhusu aya za Qur'ani nyuma ya ukurasa, ili msomaji aweze kufaidika kwa wakati mmoja kutoka kwa maandishi na maana yake," aliongeza.
4235018