Pezeshkian aliongeza kuwa juhudi ni muhimu kuandaa hija ya kila mwaka ya Arbaeen bila matatizo yoyote.
Aliyasema hayo katika mkutano wa Jumamosi wa Makao Makuu ya Arbaeen ya Iran, ambao ulihudhuriwa na wawakilishi wa mashirika tofauti yanayohusiana.
Pezeshkian alisema amekuwa na wasiwasi kwamba mabadiliko ya serikali yanaweza kusababisha matatizo katika maandalizi ya msimu wa Arbaeen, lakini ripoti zilizowasilishwa kwake ziliondoa wasiwasi wake.
Vyombo na mashirika yote yanayoshiriki katika kuandaa maandamano ya Arbaeen lazima yafanye kila liwezalo ili kutimiza ahadi zao kwa njia bora zaidi, rais alisisitiza.
Pia alisema kuwa shughuli nyingi zinazohusiana na maandamano ya Arbaeen zinafanywa na watu wenyewe, na serikali ina jukumu la kusaidia na kuhifadhi.
Kwingineko katika maelezo yake, Pezeshkian alielezea tukio la Arbaeen kama fursa ya kukuza utamaduni wa kutafuta ukweli na haki.
Kila mtu ajaribu kueneza mkabala unaotawala uasi wa Imam Hussein (AS), ambao ulikuwa ukitafuta ukweli na uadilifu, aliendelea kusema.
Maadhimisho ya Arbaeen hufanyika siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye aliuawa shahidi na jeshi katili la la Yazid katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa na 680 Miladia.
3489363
Kila mwaka mamilioni ya Mashia na pia idadi ya wasiokuwa Mashia humiminika Karbala, mji ulipo Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) kufanya ibada za maombolezo. Wafanya ziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri mamia ya kilomita kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Karbala.