IQNA

Arbaeen katika Qur’ani /2

‘Arbaeen’ imetumika katika Qur’an kuhusu Miqat ya Musa, Kukwama kwa Bani Israil

8:49 - August 18, 2024
Habari ID: 3479292
IQNA – Neno Arbaeen (maana ya siku arubaini) limetajwa ndani ya Qur’ani Tukufu kuhusu Miqat ya Musa (AS) na kuhusu jinsi Bani Isra’il walivyokwama. Kuna aya 4 ndani ya Qur’ani Tukufu ambamo Arbaeen imetajwa, 3 kati yake ni kuhusu Bani Isra’il.

Ama kuhusu Musa (AS), Quran inasema katika Aya ya 51 ya Sura Al-Baqarah: “*Na tulipo muahidi Musa masiku arubaini, kisha mkachukua ndama (mkamuabudu) baada yake, na mkawa wenye kudhulumu..”

Katika Surah Al-Aaraf, hata hivyo, Mwenyezi  Mungu anaeleza kwamba kwanza kulikuwa na kukaa kwa usiku 30 kwenye Mlima Sinai (pia unajulikana kama Jabal Musa) kwa ajili ya kuteremsha Taurati na aya za Mwenyezi Mungu na kisha kukamilishwa kwa nyongeza ya masiku kumi: “*Tulimuahidi Musa masiku thalathini na tukayatimiza kwa kumi; ikatimia miadi ya Mola wake Mlezi masiku arubaini. Na Musa akamwambia nduguye Haarun: Shika mahala pangu kwa watu wangu na utengeneze wala usifuate njia ya waharibifu. “ (Aya ya 142 ya Surah Al-A’araf)

Hii inaonyesha kwamba kumwabudu Mungu kwa siku arubaini kunaweza kuwa na matokeo maalum.

Nambari 40 pia imetajwa kuhusu adhabu ya Mwenyezi Mungu. Kwa mfano, wakati wa utume wa Nuhu (AS) ilinyesha kwa muda wa siku arubaini kuwaadhibu makafiri. Pia inasemekana kwamba kutokana na baadhi ya madhambi, Swalah ya mtu haikubaliwi kwa muda wa siku arobaini.

Vile vile tunasoma katika Surah Al-Ma’idah kwamba Bani Isra’il walijihusisha na dhambi na ili kutakaswa na kustahiki kuingia katika Ardhi Takatifu, walikwama kwa muda wa miaka arobaini. “ (Mwenyezi Mungu) akasema: Basi nchi hiyo wameharimishiwa muda wa miaka arubaini, watakuwa wakitanga-tanga katika ardhi. Basi wewe usiwasikitikie watu wapotovu.” (Aya ya 26 ya Sura Al-Ma’idah).

Kwa hakika, walifungiwa katika nchi hiyo kwa muda wa miaka arobaini kama upatanisho wa dhambi zao.

3489502

Habari zinazohusiana
Kishikizo: arbaeen qurani tukufu
captcha