IQNA

Arbaeen 1446

Maqari wa Iran hadi sasa wameandaa vikao 650 vya Qur'ani wakati wa Arbaeen

13:52 - August 23, 2024
Habari ID: 3479313
IQNA - Wajumbe wa msafara wa Qur'ani wa Iran hadi sasa wameandaa programu 650 tofauti kwa wafanyaziara wa Arbaeen nchini Iraq.

Wajumbe wa msafara huo wameandaa vikao  650 vya Qur'ani zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya siku ya Arbaeen, Seyed Mohammad Moojani, Mkuu wa Kamati ya Qur'ani ya Makao Makuu ya Arbaeen ya Iran, aliiambia Shirika la Habari la Qur'ani la Kimataifa, IQNA, siku ya Ijumaa.

Alisifu idadi ya program hizo za Qur'ani n kusema ni "muhimu na kubwa." Alibainisha kuwa data hiyo inajumuisha halka  60 za kusoma Qur'ani za maqari wa kike. "Kutokana na kukaribishwa vyema kwa programu zinazofanywa na wanawake, idadi ya wanachama wa kike wa msafara itaongezeka katika miaka ijayo," alisema.

Msafara huo wa Qur'ani wa Arbaeen unajumuisha Wairani 98 na raia wa kigeni 34 kutoka nchi 14, kama vile Afghanistan, Tajikistan, Nigeria, India na Pakistan.

Shughuli za msafara huo zitadumu kwa siku 12, Moojani alisema mapema. Mjumuiko wa maombolezo ya Arbaeen ni mojawapo ya mikusanyiko mikubwa ya kidini duniani.

Maadhimisho ya Arbaeen hufanyika siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu  wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye aliuawa shahdi na jeshi katili la la Yazid katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa na 680 Miladia.

Kila mwaka mamilioni ya Mashia na pia idadi kubwa ya wasiokuwa Mashia humiminika  katika mji Karbala nchini Iraq, mji ulipo Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) ili kushiriki katika shughuli za maombolezo. Wafanya ziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri mamia ya kilomita kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Karbala. Arbaeen ya mwaka huu inatarajiwa kuanguka mnamo Agosti 25, kulingana na kuonekana kwa mwezi.

Harakati ya mapambano ya Imam Hussein (AS) dhidi ya dhulma na ufisadi wa utawala wa Bani Umayya ilijaa hamasa, kujitolea na kusabilia kila kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, haki na uadilifu, na kwa sababu hiyo imegusa sana nyoyo za Waislamu na hata wapenda haki na kweli wasio Waislamu. Harakati hiyo ya Imam Hussein (AS) inaendelea kuibua vuguvugu na hamasa ya aina yake ndani ya nafsi za wapenzi wa mtukufu huyo.

3489620

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: arbaeen qurani tukufu
captcha