IQNA

Arbaeen 1446 H

Msafara wa Qur’ani wa Iran wa Arbaeen wakamilisha Shughuli baada ya Kufanya Programu 1,000 nchini Iraq

23:41 - August 26, 2024
Habari ID: 3479331
IQNA - Msafara wa Qur'ani wa Iran uliotumwa Iraq kushiriki katika vikao vya Qur'ani kwa munasaba wa Arbaeen ulihitimisha shughuli zake baada ya karibu siku kumi.

Wanachama wa msafara huo waliondoka katika mji mtakatifu wa Najaf kuelekea Iran Jumapili jioni.

Seyed Mohammad Mojani, mkuu wa kitengo cha masuala ya Qur'ani ya Kamati ya Kitamaduni na Elimu ya Makao Makuu ya Arbaeen, aliiambia IQNA kwamba ujumbe huo unaojulikana kama Msafara wa Qur'ani wa Noor, ulikuwa na wajumbe 100.

Wajumbe hao walishiriki katika vikao zaidi ya 1,000 vya Qur'ani wakati wakiwa Iraq, alisema.

Programu yao ya mwisho ya Qur'ani iliandaliwa Jumapili na kuhudhuriwa na maafisa kadhaa, akiwemo Mwambata wa Utamaduni wa Iran Gholam Reza Abazari, na afisa wa Shirika la Wakfu na Masuala ya Hisani Mohammad Mehdi Shakiba, aliongeza.

Mojani alisema Hamid Reza Ahmadivafa, Hadi Esfidani, Omid Hosseininejad na Mohammad Hassan Hassanzadeh waliosoma Qur’ani Tukufu katika hafla hiyo.

Maadhimisho ya Arbaeen hufanyika siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu  wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye aliuawa shahdi na jeshi katili la la Yazid katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa na 680 Miladia.

Kila mwaka mamilioni ya Mashia na pia idadi kubwa ya wasiokuwa Mashia humiminika  katika mji Karbala nchini Iraq, mji ulipo Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) ili kushiriki katika shughuli za maombolezo. Wafanya ziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri mamia ya kilomita kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Karbala. Arbaeen ya mwaka huu yamefanyika Agosti 25.

Harakati ya mapambano ya Imam Hussein (AS) dhidi ya dhulma na ufisadi wa utawala wa Bani Umayya ilijaa hamasa, kujitolea na kusabilia kila kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, haki na uadilifu, na kwa sababu hiyo imegusa sana nyoyo za Waislamu na hata wapenda haki na kweli wasio Waislamu. Harakati hiyo ya Imam Hussein (AS) inaendelea kuibua vuguvugu na hamasa ya aina yake ndani ya nafsi za wapenzi wa mtukufu huyo.

https://iqna.ir/en/news/3489650

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu arbaeen
captcha