IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Qur’ani Tukufu yateketezwa mara kadhaa huko Uswidi (Sweden)

22:34 - May 29, 2022
Habari ID: 3475310
TEHRAN (IQNA)- Rasmus Paludan, mwanasiasa mwenye msimamo mkali mwenye uraia wa Sweden na Denmark ambaye alizindua msafara wa kuteketeza moto Qur’ani Tukufu nchini Sweden hivi karibuni amekariri jinai yake hiyo yenye chuki dhidi ya Uislamu katika bustani ya jiji la Landskrona kusini mwa Sweden.

Paludan amekariri jinai yake hiyo Ijumaa huku akiwa analindwa na maafisa wa polisi na chama cha Stram Kurs  yaani Msimamo Mkali ambacho anakiongoza.

Paludan pia hapo awali alifanya vitendo vyake vya uchochezi dhidi ya Waislamu wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Qur'ani karibu na maeneo ya Waislamu na misikiti nchini Uswidi chini ya ulinzi wa polisi.

Kufuatia jinai hiyo, kumeibuka maandamano katika miji mbali mbali ya Sweden ikiwemo Stockholm, Linköping, Landskrona, Malmo na Norrkoping ambapo waandamanaji wamepinga vikali kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na njama ya kukariri kitendo hicho. Watu kadhaa wamejeruhiwa na magari yameteketezwa moto katika maandamano hayo. 

Nchi kadhaa za Kiislamu ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zililaani jinai hiyo na kutaka serikali ya Sweden ichukue hatua za kuzuia kukaririwa kwake.

4060349

captcha