IQNA

Waislamu Sweden

Msikiti wahujumiwa kusini mwa Uswidi

13:09 - September 10, 2022
Habari ID: 3475759
TEHRAN (IQNA) – Msikiti katika mji wa kusini mwa Uswidi (Sweden) wa Jönköping umehujumiwa na kuharibiwa kwa mara ya tatu katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Msikiti huo  unaohusishwa na Idara ya Masuala ya Kidini ya Urais wa Uturuki ulipigwa mawe katika shambulio la wenye chuki dhidi ya Uislamu, afisa mmoja alisema Ijumaa.

Mehmet Ozer, afisa kutoka Msikiti wa Jonkoping kusini mwa Uswidi, anmewwambian waandishi habari kwamba waligundua shambulio hilo walipoenda kuswali Sala ya Ijumaa.

"Tukio hilo liliripotiwa kwa polisi na mamlaka husika," Ozer aliongeza. "Hili ni shambulio la tatu kwenye msikiti wetu katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Tunawasilisha malalamiko yetu, lakini hatuna matumaini sana, kwani hatukupata matokeo yoyote kutokana na malalamiko ya awali."

Ozer alisema kuwa dirisha la jikoni la msikiti huo, unaohusishwa na Wakfu wa Diyanet wa Uswidi, lilivunjwa katika shambulio hilo, na wanashuku kuwa shambulio hilo lilifanywa kwa sababu za ubaguzi wa rangi.

3480409

captcha