IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Mwanasiasa aliyevunjia heshima Qur'ani Tukufu Uswidi ahukumiwa

16:15 - November 06, 2024
Habari ID: 3479709
IQNA - Mwanasiasa wa siasa kali za mrengo wa kulia wa Denmark amehukumiwa kifungo cha miezi minne jela na mahakama ya Uswidi kwa kuchochea chuki za kikabila kwa kuchoma moto Qur'ani Tukufu.

Rasmus Paludan, kiongozi wa chama cha mrengo mkali wa kulia cha Stram Kurs (Msimamo Mkali) cha Denmark, ndiye mtu wa kwanza kupatikana na hatia ya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu nchini Uswidi.
Hukumu hiyo inahusiana na maandamano huko Malmo mnamo 2022 ambapo Paludan alichoma Qur'ani Tukufu na kutoa matamshi ya dharau kuhusu Waislamu.
Mahakama ya Wilaya ya Malmo ilisema kuwa Paludan alifunga nakala ya Qur'ani kwenye nyama ya nguruwe na kuichoma moto huku akitumia lugha iliyoonekana kuwakera Waislamu.
Vitendo vyake vilizingatiwa kukiuka ukosoaji unaoruhusiwa wa umma na mazungumzo ya kuwajibika, kulingana na Jaji Nicklas Soderberg.
Ushenzi wa Paludan nchini Uswidi mnamo 2022, wakati wa likizo ya Pasaka, ulijumuisha uchochezi sawa huko Malmo, Norrkoping, Jonkoping, na Stockholm, na kusababisha machafuko yaliyoenea. Matukio haya yalijeruhi maafisa wa polisi 104 na waandamanaji 14, na uharibifu mkubwa kwa magari ya polisi.
Kuchomwa kwa nakala ya Qur'ani Tukufu nje ya ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm Januari 2023 kulivuruga uhusiano wa kidiplomasia wa Uswidi na kuathiri jitihada zake za NATO. Denmark baadaye ilipitisha sheria mnamo Desemba 2023 ya kupiga marufuku kunajisi maandishi ya kidini, na adhabu ikiwa ni pamoja na faini au kifungo cha hadi miaka miwili jela.

3490581

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu uswidi
captcha