IQNA

Siku tatu za maombolezo ya kitaifa Iran kwa ajili ya waliouawa katika ghasia zilizochochewa na Marekani, Israel

14:40 - January 12, 2026
Habari ID: 3481792
IQNA-Serikali ya Iran imetangaza siku tatu za maombolezo kwa ajili ya kuwakumbuka waathiriwa, wakiwemo askari wa vikosi vya usalama na wa jeshi la kujitolea, ambao wameuliwa shahidi na magaidi wafanyaji fujo na vurugu wanaoungwa mkono na Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel, waliojaribu kuteka nyara maandamano ya amani ya wananchi ya kulalamikia hali ya uchumi nchini.

Serikali imetoa tangazo hilo katika taarifa siku ya Jumapili, iliyozifananisha vurugu hizo mbaya za mauaji na umwagaji damu na jinai za kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS).

"Rais na serikali watakaa kuwaomboleza mashahidi wapendwa wa Iran," imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ya serikali imeeleza kwamba, Mashahidi hao walijitolea maisha yao katika njia ya "Muqawama wa kitaifa wa Wairani kukabiliana na Marekani na utawala wa Kizayuni."

Vilevile, imebainisha kuwa waathiriwa hao ni pamoja na askari wa vikosi vya jeshi la polisi la Jamhuri ya Kiislamu na wa jeshi la kujitolea la Basij.

"Taifa la Iran lilmehisi kwa dhati jinsi watenda jinai walivyowaathiri wananchi wapendwa, wakiwemo askari wa Basij na wa vikosi vya polisii, na kuwaua shahidi watu wengi wapendwa," imeongezea kueleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya serikali hadi sasa, vurugu kama hizo zimeshuhudiwa kufanywa na magaidi wa Daesh tu wanaolelewa na Marekani.

Taarifa hiyo ya serikali imetolewa kufuatia mauaji ya kinyama ya raia kadhaa wa Iran na maafisa wa usalama yaliyofanywa na wazushaji vurugu na machafuko, ambao wamethibitishwa na vyombo vya intelijensia vya Jamhuri ya Kiislamu kwamba walikuwa wakipokea misaada ya kijasusi, ya kioperesheni, ya vifaa, na kifedha kutoka Washington na shirika la ujasusi la utawala haramu wa Israel, Mossad.

Kauli ya Rais Pezeshkian

Wakati huo huo, Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, adui amewaingiza Iran magaidi waliopewa mafunzo maalumu ya kigaidi ili kufanikisha malengo yake na kwamba waliofanya fujo, machafuko na uharibifu katika kona mbalimbali za Iran, si katika wananchi waliokuwa wanaandamana.

Rais Pezeshkian alisema hayo jana Jumapili wakati alipozungumza na wananchi kwa njia ya televisheni na kusema: Adui amewaingiza humu nchini magaidi waliopata mafunzo maalumu lengo likiwa ni kushadidisha machafuko na ukosefu wa amani nchini.

Amesema kwamba jukumu la serikali ni kutatua matatizo na kundoa wasiwasi wa wananchi; na zaidi ya hilo serikali ina wajibu wa kutotoa mwanya kwa wafanya machafuko kuivuruga nchi; na kwamba familia zisiwaruhusu vijana wao kujiingiza katika ghasia za magaidi hao. Rais Pezeshkian ameeleza haya ikiwa ni majibu yake kuhusu matukio ya hivi karibuni ya machafuko humu nchini. 

Vilevile ameashiria maandamanao ya siku za karibuni ya wafanyabiashara na kuongeza kuwa: Katika kikao na pande mbili hizo kati ya Serikali na wafanyabiashara, serikali imesikiliza daghadagha na malalamiko yao na imeshaanza kuchukua hatua za kutatua changamoto hizo. Kwenye kikao hicho baina ya serikali na wafanyabiashara kulichukuliwa maamuzi muhimu ya kuyapatia ufumbuzi matatizo ya tabaka hilo katika jamii. Hii ni kwa sababu serikali inataka kutatua matatizo yao kadiri inavyowezekana.

Aidha Rais Pezeshkian amesisitiza kuwa, adui katika vita vya siku 12 pia alikusudia kuitumbukiza Iran katika machafukoni na kwamba maadui wa wananchi wa Iran hii leo pia wameazimia kushadidisha vurugu ili wapate mwanya wa kuingilia zaidi masuala ya ndani ya nchi hii. 

3496038

captcha