
Rais Pezeshkian amesema hayo katika mazungumzo yake ya simu na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambapo alitoa shukrani zake kwa misimamo imara, yenye kanuni, na ya kidugu ya serikali na watu wa Uturuki katika kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Akizungumzia kuhusika moja kwa moja Marekani na utawala wa Kizayuni katika matukio haya, Rais Pezeshkian amesema: "Maandamano yaliyoanzishwa na baadhi ya wafanyabiashara wa soko na vyama vya wafanyakazi kufuatia matatizo ya kiuchumi yanayotokana na mashinikizo na vikwazo vikali yalikuwa ndani ya mfumo wa amani kabisa na kwenye njia ya usimamizi na utatuzi, lakini makundi ya magaidi waliofunzwa, walifanya vitendo visivyo vya kawaida kama vile kuchoma moto misikiti, vituo vya umma na serikali, kuharibu vifaa na zana za misaada, na pia kuwaua watu shahidi na vikosi vya usalama na vya kutekeleza sheria, kwa usaidizi wa moja kwa moja wa Marekani na utawala wa Kizayuni, walikuwa wakitafuta kufikia malengo yao ya uharibifu. Hata hivyo, njama hizi zilivunjwa kwa mahudhurio ya mamilioni ya Wairani waliojitokeza na kulaani vitendo hivyo vya magaidi.
Habari inayohusiana:
Rais wa Iran amesema kuwa, ana uhakika kwamba kwa umoja, mshikamano, na mitazamo ya pamoja ya nchi za ulimwengu wa Kiislamu na juhudi na mapambano yote dhidi ya tukio baya la ugaidi, eneo hilo litaelekea kwenye amani, utulivu, na usalama wa kudumu.
Katika sehemu nyingine ya mazungumzo yake na Rais wa Uturuki, Dkt. Pezeshkian, ameelezeakiwango bora na kinachohitajika sana cha uhusiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jamhuri ya Uturuki, na kubainisha kwamba: "Uhusiano kati ya nchi hizo mbili uko katika njia nzuri sana na tumeazimia kuimarisha zaidi uhusiano wa pande mbili.
4329761