kiislamu - Ukurasa 3

IQNA

Rais Hassan Rouhani wa Iran
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ulimwengu wa Kiislamu una changamoto nyingi kitaifa na kimataifa na kusisitiza kuwa, nchi za Kiislamu zinapaswa kuwa na tadibiri na mikakati madhubuti ya kuachana na ubeberu wa sarafu ya dola wa kutegemea mfumo wa kifedha wa Marekani.
Habari ID: 3472287    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/19

TEHRAN (IQNA)- Shirika moja la kiteknolojia nchini Malaysia limefanikiwa kutegeneza browser ya kwanza duniani ambayo inaenda kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu kwa lengo la kuwahudumia Waislamu bilioni 1.8 duniani ili waweze kuwa na mazingira halali na salama katika intaneti.
Habari ID: 3471996    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/12

TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Ethiopia wanaendelea kunufaika na huduma za Kiislamu katika taasisi za kifedha nchini humo.
Habari ID: 3471901    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/06

TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Kimataifa ya Maulama wa Kiislamu imelaani vikali mkutano wa hivi karibuni baina ya maafisa wa ngazi za juu wa nchi za Kiarabu na Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni wa Israel huko Warsaw, Poland.
Habari ID: 3471846    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/02/19

TEHRAN (IQNA)-Jengo la Taj Mahal nchini India, moja kati ya Maajabu Saba ya Dunia, na ambalo huwavutia watalii wasiopungua milioni sita kwa mwaka limeondolewa katika orodha ya vivutio vya kitalii kwa sababu ni turathi ya Kiislamu.
Habari ID: 3471210    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/10/10

TEHRAN (IQNA)-Sherehe ya kuidhinisha kura za wananchi kwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu zimefanyika leo hapa Tehran kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kumuidhinisha Hassan Rouhani kuwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3471101    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/08/03

TEHRAN (IQNA)-Wakuu wa vyuo vikuu vya nchi za Kiislamu wamekutana Ankara, mji mkuu wa Uturuki na kujadili kuundwa Baraza Kuu la Kiislamu la Ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3471091    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/07/27

TEHRAN (IQNA)-Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya Jijja ametoa wito kwa Waislamu wasiibue masuala ya hitilafu za kimadhehebu katika Ibada ya Hija.
Habari ID: 3471087    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/07/26

TEHRAN (IQNA)-Taasisi za Kiislamu Palestina zimechukua hatua za pamoja kupinga vizingiti vilivyowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Msikiti wa al-Aqsa.
Habari ID: 3471084    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/07/25

TEHRAN (IQNA)-Waalimu wa shule za Kiislamu (Madrassah) nchini Uganda wameshiriki katika warsha ya kuimarisha ujuzi wao.
Habari ID: 3471083    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/07/24

TEHRAN (IQNA)-Zakir Naik, mhubiri wa Kiwahhabi mwenye utata amepokonywa pasi yake ya kusafiria na serikali ya India.
Habari ID: 3471075    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/07/19

TEHRAN (IQNA)-Mmoja kati ya misikiti ya kale zaidi nchini Kenya uko katika hatari ya kuangamia kutokana na ongezeko la mawimbi ya bahari.
Habari ID: 3471068    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/07/15

TEHRAN (IQNA)-Wataalamu wa akiolojia wamegundua mji wa kale wa Kiislamu ambao ulikuwa kituo cha kibiashara zaidi ya miaka 1,000 iliyopita
Habari ID: 3471024    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/06/18

TEHRAN (IQNA)-Mji mkuu wa Kenya, Nairobi leo ni mwenyeji wa mkutano wa siku mbili ambao unachunguza namna nchi hiyo inaweza kunufaika na uchumi wa Kiislamu au uchumi Halal ambao unashika kasi duniani.
Habari ID: 3470929    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/04/10

TEHRAN (IQNA)-Serikali ya Kenya imezindua bajeti ambayo itastawisha mfumo wa Kiislamu wa kifedha nchini humo kwa lengo la kuufanya mji mkuu, Nairobi kuwa kitovu cha sekta hiyo kieneo.
Habari ID: 3470918    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/04/04

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe wa kuanza mwaka mpya wa 1396 Hijria Shamsia akiwapongeza Wairani na Waislamu kote duniani kwa mnasaba wa siku ya kuzaliwa Bibi Fatima Zahra SA na Sikukuu ya Nowruz na ameupa mwaka mpya jina la Mwaka wa Uchumi wa Kimapambano, Uzalishaji na Ajira.
Habari ID: 3470902    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/03/20

IQNA-Jumba la Makumbusho la Qatar ambalo lina mkusanyiko mkubwa zaidi za sarafu za Kiislamu duniani limeandaa maonyesho yenye sarafu muhimu zaidi ya Kiislamu duniani.
Habari ID: 3470894    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/03/14

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
IQNA:Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa taifa la Iran litajibu vitisho vilivyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani katika maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ijumaa ijayo.
Habari ID: 3470839    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/02/07

IQNA-Mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran umezinduliwa rasmi kama Mji Mkuu wa Utamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2017.
Habari ID: 3470781    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/01/04

IQNA-Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesaini sheria itakayoimarisha nafasi ya Kenya kama kitovu cha mfumo wa fedha wa Kiislamu barani Afrika.
Habari ID: 3470779    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/01/04