IQNA

11:03 - June 12, 2019
News ID: 3471996
TEHRAN (IQNA)- Shirika moja la kiteknolojia nchini Malaysia limefanikiwa kutegeneza browser ya kwanza duniani ambayo inaenda kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu kwa lengo la kuwahudumia Waislamu bilioni 1.8 duniani ili waweze kuwa na mazingira halali na salama katika intaneti.

Kati ya sifa za browser hiyo ambayo inajulikana kama SalamWeb ni kuwa inaonyesha nyakati za sala kwa mujibu wa eneo la kijiografia aliko mtumizi na pia ina dira ya kuonyesha qibla.

Hali kadhalika browser (kivinjari wavuti) ya SalamWeb inatoa tahadhari wakati unapojaribu kuingia katika ukurasa wa intaneti wenye maudhui zinazokinzana na maadili ya Kiislamu.

Browser hiyo imetayarishwa kwa lugha kadhaa na ina muundo sahali mbali na kumuwezesha mtumizi kuongeza aplikesheni ambazo zinaenda kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.  SalamWeb inaweza kutumiwa kwa lugha kadhaa ikiwemo lugha ya Kiswahili na hivyo kuwawezesha Waislamu wa maeneo yote duniani kunufaika na huduma zake.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la SalamWebTechnologise Hajjah Hasni Zarina anasema vijana Waisalmu wa kizazi cha sasa ambao wanafungamana na imani ya Kiislamu na wanapenda teknolojia wamekuwa wakitafuta suluhisho la kivitendo ambalo linaweza kukidhi mahitaji yao.

Anasema kwa kuzingatia kuwa Waislamu bilioni 1.8 ni asilimia 24 ya watu wote duniani, shirika hilo ambalo lina makao makuu yake Kuala Lumpur, Malaysia limehisi kuna fursa kubwa ambayo inapaswa kutumiwa ili kuwawezesha Waislamu kutumia teknolojia halali.

Aidha amebaini kuwa ingwa browser hiyo imetayarishwa kwa kutegemea mafundisho ya Kiislamu, mtu yeyote anaweza kutumia bila kujali itikadi yake.

Shirika la Malaysia latengeneza browser ya kwanza ya Kiislamu duniani

3818655

Name:
Email:
* Comment: