Maelfu ya wanaharakati wa kundi la Ikhwanull Muslimin na wafuasi wao walifanya maandamano ya nchi nzima baada ya sala ya Ijumaa wakipinga ukandamizaji mkubwa unaofanywa na jeshi lililompindua rais huyo aliyechaguliwa na wananchi mwezi Julai mwaka huu.
Katika maandamano hayo ya jana wafuasi wa Mosri walitaka kurejeshwa madarakani rais huyo wa Misri na kuachiwa huru wanaharakati wa Ikhwan waliotiwa mbaroni na polisi.
Serikali ya Misri iliyowekwa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi imeitangaza Ikhwanul Muslimin kuwa ni kundi la kigaidi, katika hatua ya utekelezaji ramani ya njia iliyoandaliwa tangu yalipofanyika mapinduzi hayo dhidi ya Muhammad Morsi, rais halali wa nchi hiyo.
Muhammad Morsi, rais halali wa Misri aliondolewa madarakani tarehe 3 Julai mwaka huu kupitia mapinduzi ya kijeshi. Na kuanzia wakati huo ikaanza kampeni ya kuchukua hatua dhidi ya viongozi na wanachama wa Ikhwanul Muslimin kwa kuwatia nguvuni na kuwaweka korokoroni.
132376