Sherehe za ufunguzi zimehudhuriwa na wageni waheshimiwa akiwemo Mkuu wa Vyombo vya Mahakama katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Amoli Larijani, na Hujjatul Islam wal Muslimin Mohammadi Golpaygani ambaye ni Mkuu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Hafla hiyo ilianza kwa qiraa ya Qur'ani Tukufu na kufuatiwa na hotuba ya Hujjatul Islam wal Muslimin Ali Mohammadi Mkuu wa Idara ya Awqaf Iran ambayo inasimamia mashindano hayo.
Katika hotuba yake alisema mashindano ya mwaka huu ambayo yatamalizika Juni pili yana maqarii na mahufadh 120 wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi 75 duniani huku kukiwa na jopo la majaji 15 ambapo 10 kati yao ni kutoka nchi za kigeni na watano ni Wairani.
Hujjatul Islam wal Muslimin Ali Mohammadi alisema siri ya kupatikana umoja katika ulimwengu wa Kiislamu ni uzingatiwaji mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
1411407