IQNA

Ibada

Mosalla Tehran kupanuliwa ili kuwa msikiti mkubwa zaidi duniani

9:48 - February 27, 2025
Habari ID: 3480275
IQNA-Eneo kubwa la Swala la Tehran maarufu kama Mosalla Imam Khomeini litapanuliwa na kuwa msikiti mkubwa zaidi duniani.

Afisa mwandamizi wa kitengo cha ujenzi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), kinachojulikana kama Makao Makuu ya Khatam, amesema Jumatano kuwa Msikiti wa Mosalla utapanuliwa kwa hekta 200 kutokana na miradi ya inayoendelea hivi sasa

Mohammad Reza Rahmani, ambaye anaongoza kitengo cha usafiri na maendeleo ya miji cha Khatam amesema kwa vipimo hivi, Msikiti wa Mosalla utakuwa na eneo kubwa zaidi la Swala duniani. Amesema mradi huo pia utajumuisha majengo kadhaa ya shughuli za kidini na kiutamaduni.

Rahmani alisema kuwa Msikiti Mkuu wa Mosalla wa Tehran utaunganishwa na eneo kubwa la kijani katika kaskazini mwa Tehran, linalojulikana kama Chahar Bagh, kupitia daraja la lililojengwa juu ya Barabara ya Shahid Soleimani.

Amesema kuwa muunganisho huo utapanua eneo linaloweza kufikiwa la msikiti, na kuwapa waumini vivutio zaidi, ikiwa ni pamoja na maeneo zaidi ya maegesho..

Afisa huyo amesema kuwa ardhi zaidi katika eneo la Abbas Abad mjini Tehran zitanunuliwa na serikali ili kupanua eneo linalotumika la Mosalla

Ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Mosalla wa Tehran ulianza mapema miaka ya 1980 kwa pendekezo la viongozi wa kidini kwa lengo la kubadilisha mahali pa Swala ya Ijumaa ya Tehran kutoka Chuo Kikuu cha Tehran hadi eneo pana.

Mradi huo baadaye ulipanuka na kuwa jumuiya kubwa ya kitamaduni, yenye kumbi ambazo  huwa mwenyeji maonyesho makubwa ya kila mwaka na sherehe za kidini katika kituo hicho.

/3492065

Kishikizo: mosalla tehran msikiti
captcha