Sayed Fadhl al-Sharafi alitoa kauli hiyo katika hotuba yake kwenye Maonyesho ya 32 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran.
Alikuwa akihutubia jukwaa lenye mada "Harakati za Mazungumzo Kati ya Vijana wa Ulimwengu wa Kiislamu", lililofanyika kwenye maonyesho hayo siku ya Jumamosi jioni.
Msomi huyo alisisitiza umuhimu wa Waislamu kushikamana na mafundisho ya Qur'an Tukufu na Ahl-ul-Bayt (AS).
Alizungumzia mwezi mtukufu wa Ramadhani, akibainisha kuwa huu ni mwezi ambao Quran Tukufu iliteremshwa ili kuwaongoza watu.
Amesema kuwa matukio kama Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani yanayofanyika mjini Tehran, ambayo yanalenga kukuza mwonekano wa kidhahiri wa Qur'an na mafundisho yake, ni mifano ya kuonyesha umuhimu wa Qur'ani.
Hata hivyo, alisisitiza kuwa ni muhimu kuzingatia maudhui ya Qur'ani na ujumbe wake wa kina.
Msomi huyo wa kidini alieleza umuhimu wa kuhifadhi na kusoma Qur'ani kwa usahihi, pamoja na umuhimu wa uchapishaji wake na sanaa ya uandishi wake.
Al-Sharafi alibainisha kuwa ingawa juhudi hizi zinaonyesha heshima kubwa kwa Quran, ni muhimu vilevile kuelewa maana na malengo yake ya kina.
Aliikosoa jamii zinazoonekana kuthamini Qur'an lakini kwa matendo zinakengeuka kutoka katika kanuni zake. Alitoa mfano wa makundi ya kigaidi kama Daesh (ISIL au ISIS) ambayo, ingawa yanadai kueneza mafundisho ya Qur'ani, yanahusika katika uhalifu wa kikatili, ikiwa ni pamoja na mauaji ya Waislamu huko Yemen na katika nchi nyingine za Kiislamu.
Al-Sharafi aliongeza kuwa Qur'ani ina malengo muhimu, kama vile Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ni muhimu kutilia maanani dhana hizi.
Alisisitiza kuwa umakinifu kwa Qur'ani unapaswa kuwa wa uwiano, yaani, kushughulikia mwonekano wake wa nje pamoja na maudhui yake ya ndani kwa wakati mmoja, ili Waislamu waweze kunufaika ipasavyo na mafundisho yake na kuyafanikisha malengo yake makuu.
Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'an Tukufu yanaendelea katika ukumbi wa Mosalla Imam Khomeini (RA) mjini Tehran, kwa heshima ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
3492244