IQNA

Ni haramu kuyaunga mkono makundi ya kigaidi

16:15 - September 08, 2014
Habari ID: 1448164
Mufti Mkuu wa Misri, Shawki Ibrahim Abdel Karim Allam amesema kuwa, ni haramu kuunga mkono makundi ya kigaidi.

Mufti Allam amelaani jinai za ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati na kusema kuwa umefika wakati wa walimwengu wote kuunganisha nguvu zao ili kukabiliana na wimbi la makundi ya kigaidi. Amelaani pia mashambulizi ya kigaidi ambayo yamekuwa yakifanywa katika eneo la Sinai nchini Misri na kusema kuwa, magaidi hawana nia nyengine ghairi ya kuzusha machafuko katika nchi, kudhoofisha usalama na kuzishughulisha fikra za wananchi ili wasahau masuala muhimu yanayoikabili dunia ya leo. Amesema kuwa, kuwasaidia magaidi kwa aina yoyote ile ni haramu na mtu yeyote anayefanya jambo hilo anakuwa mshirika katika dhambi.
Hivi karibuni pia Mufti Mkuu wa Misri alionya juu ya hatari kubwa ya kundi la kitakfiri la Daesh huko nchini Iraq na Syria. Alisema kuwa, kundi la Daesh ni tishio kubwa kwa dini tukufu ya Kiislamu na Waislamu na amewataka Waislamu kujiepusha na kundi hilo.

  1446183

Kishikizo: Mufti, Misri, ugaidi, daesh
captcha