IQNA

'Kuna hamu ya Uislamu barani Ulaya'

22:28 - September 30, 2014
Habari ID: 1455969
Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya Hija amesema kuwa, kwa vile kiwango cha mwelekeo na hamu juu ya dini ya Kiislamu imeongezeka barani Ulaya, viongozi wa bara hilo wanaamini kwamba Uislamu utaweza kulikamata bara hilo katika siku za usoni.

Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Ali Qadhi Asghar ameyasema hayo jana kwenye kongamano la kuzikurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu mjini Makka na kusema kwamba Uislamu ni dini ya ulimwengu na ina miongozo sahihi katika shughuli zote za maisha ya mwanadamu. Qadhi Asghar amesisitiza kuwa, iwapo mahubiri na mafundisho ya Kiislamu yatafikishwa kwa njia sahihi kwa walengwa, bila shaka makundi kwa makundi ya walimwengu yataikubali na kuifuata dini hiyo tukufu. Akielezea kwamba hakuna sababu zozote za kuibuka hitilafu kati ya Waislamu, Sayyid Qadhi Asghar amesema kuwa, leo hii maadui wa dini ya Kiislamu wanafanya njama za kuzusha hitilafu na mifarakano kati ya wafuasi wa madhehebu mbalimbali, kwa lengo la kupora maliasili na utajiri wa nchi za Kiislamu. Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya Hija amewataka wanafikra, wasomi na waandishi kuwatanabaisha Waislamu na masuala yanayoweza kuzusha fitina na hitilafu kati yao.../mh

1455814

captcha