IQNA

Kadhia ya Palestina

Maelfu wahudhuria Kongamano la Wapalestina Barani Ulaya

16:56 - May 28, 2023
Habari ID: 3477060
TEHRAN (IQNA) – Toleo la 20 la Kongamano la Wapalestina Wanaoishi Ulaya lilifanyika Malmo, Uswidi, Jumamosi. Maelfu ya Wapalestina wanaoishi katika nchi za Ulaya walishiriki katika mkusanyiko huo, Al-Ahed News iliripoti.

Pia waliohudhuria ni viongozi wa kisiasa na mashirika ya kiraia, wakiwemo wabunge, wanaharakati wa haki za binadamu na wanahabari kutoka Uswidi (Sweden), Italia na Ireland.
Kongamano hilo lilikuwa na vikao tisa, vikiwemo vya vijana na wanawake.
Pembezoni mwa kongamano hilo, matukio kadhaa kama vile maonyesho, matukio ya sanaa, warsha na matamasha yalifanyika kwa lengo la kuangazia masuala yanayohusiana na Palestina."Miaka 75 ... Tutarudi" ilikuwa kauli mbiu ya kongresi, ambayo ilisisitiza haki ya kurudi kwa Wapalestina wote. Kongamano hilo ambalo limefanyika kwa miongo miwili huvutia maelfu ya Wapalestina kila mwaka.
Uswidi ina idadi kubwa ya pili ya Wapalestina barani Ulaya.

4144112

Kishikizo: palestina ulaya
captcha