IQNA

Jumuiya ya Wanazuoni wa Qum: Sheikh Nimr aachiwe huru

9:51 - October 17, 2014
Habari ID: 1460866
Jumuiya ya Wanazuoni na Wakufunzi wa Chuo Kikuu cha Kidini cha mji mtakatifu wa Qum nchini Iran imelaani hukumu ya kifo iliyotolewa na mahakama moja ya Saudi Arabia dhidi ya mwanazuoni mkubwa wa nchi hiyo Ayatullah Nimr Baqir al Nimr na imetoa wito wa kuachiwa huru msomi huyo bila ya masharti yoyote.

Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Wanazuoni na Wakufunzi wa Qum imesema kuwa Waislamu wanaodhulumiwa wa madhehebu ya Shia katika ardhi ya Hijaz (Saudi Arabia) wananyimwa haki ndogo kabisa za mwanadamu kama uhuru wa kujieleza na wanastahamili dhulma na ukandamizaji mkubwa wa watawala wa kifalme wa Aal Saud huku nchi zinazodai kutetea haki za binadamu zikiendelea kutia pamba masikioni.
Taarifa ya jumuiya hiyo imelaani vikali hukumu ya kifo dhidi ya Sheikh Nimr wa Saudi Arabia na kusema imeamsha hasira za raia na maulamaa wa nchi hiyo.
Ayatullah Nimr Baqir al Nimr ni msomi na mpigania haki za binadamu wa Saudi Arabia ambaye alitiwa nguvuni na vyombo vya usalama vya utawala wa Riyadh kufuatia harakati na maandamano ya Waislamu wanaokandamizwa wa madhehebu ya Shia nchini humo mwaka 2012. Juzi Jumatano mahakama moja ya Saudi Arabia ilimhukumu kifo msomi huyo kwa kosa eti la uchochezi na kutomtii mfalme wa nchi hiyo. 

  1460797

captcha