IQNA

Kanali ya televisheni ya satalaiti ya "Kuamrisha Mema na Kukataza Maovu" kufunguliwa Saudi Arabia

11:54 - November 05, 2008
Habari ID: 1704816
Mkurugenzi Mkuu wa Kamati ya Kuamrisha Mema na Kukataza Mabaya ya Makka Ahmad al Ghamidi amesema kuwa kanali ya televisheni ya Kuamrisha Mema na Kukataza Maovu itaanzishwa nchini huyo.
IQNA imenukuu gazeti la al Riyadh kwamba Sheikh Ahmad al Ghamidi amesema, mradi wa kuanzisha kanali hiyo ya televisheni unafanyiwa uchunguzi. Amesema kuwa lengo la kuanzishwa kanali hiyo ni kutumia teknolojia ya kisasa kwa ajili ya kuwaelimisha Waislamu wa Saudi Arabia misingi ya Uislamu na kuimarisha mafunzo ya maadili bora katika jamii.
Al Ghamidi amesema, kuanzishwa kwa kanali hiyo ya telesheni ya satalaiti kutaiwezesha Kamati ya Kuamrisha Mema na Kukataza Maovu ya Saudi Arabia kuwa na mipango bora zaidi ya kuwaelimisha raia.
Ni vema kukumbusha hapa kuwa suala la kuanzishwa televisheni ya satalaiti ya Kuamrisha Mema na Kukataza Maovu huko Saudi Arabia imepasishwa na washiriki katika kikao cha tatu cha kamati hiyo katika mji wa al Khubar, mashariki mwa Saudi Arabia. 315591
captcha