IQNA

Saaza za kutembelea Kituo cha Kuchapisha Qur’ani cha Madina

18:00 - May 23, 2026
Habari ID: 3482272
IQNA – Wageni wanaozuru mji mtukufu wa Madina katika kipindi cha Hija ya mwaka 1447 (2026) watapata fursa ya kutembelea Kituo cha Mfalme Fahd cha Kuchapisha Qur’ani Tukufu katika nyakati maalum zilizotangazwa hivi karibuni.

Kituo hicho kitakuwa wazi kwa ajili ya wageni kuanzia siku ya Jumapili hadi Alhamisi, ambapo vipindi vya ziara vimegawanywa katika sehemu mbili:

  • Kipindi cha kwanza: Kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.
  • Kipindi cha pili: Kuanzia saa 8:00 mchana hadi saa 1:00 usiku.

(Hakuna taarifa zilizotolewa kuhusu siku ya Ijumaa na Jumamosi).

Kituo hiki, ambacho kilianzishwa mwaka 1984, ndicho kituo kikubwa zaidi duniani cha uchapishaji na usambazaji wa Qur’ani Tukufu. Kituo hiki huzalisha takriban nakala milioni 10 za Qur’ani kila mwaka, zikiwemo tafsiri katika lugha nyingi kama vile Kiingereza, Kiindonesia, Kirusi, Kijapani, Kiajemi, Kiurdu, Kibengali, na Kikorea.

Dhumuni kuu la kituo hiki ni kuchapisha na kusambaza nakala za Qur’ani kwa kuzingatia qiraa zilizothibiti (Mutawatir). Aidha, matoleo ya kidijitali na ya sauti ya Qur’ani yanapatikana kwa ajili ya mahitaji ya wote wanaohitaji, kupitia mifumo ya kielektroniki na programu za simu janja (smart applications).

3497531

captcha