IQNA

Maonyesho ya nakala za maandiko ya mkono ya Kiislamu huko Durban, Afrika Kusini

14:10 - November 06, 2008
Habari ID: 1705164
Maonyesho ya nakala za maandishi ya kale ya mkono yamefunguliwa katika mji wa Durbar nchini Afrika Kusini kwa shabaha ya kuchunguza historia ya Kiislamu.
Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Mali Pallo Jordan amesema katika sherehe za ufunguzi wa maonyesho hayo kwamba maonyesho hayo yamekusanya nakala za maandishi ya mkono ya kale ya karne ya 13 hadi 19 Miladia kutoka nchi zote za Afrika kwa shabaha ya kutazama na kutathmini historia na utajiri wa utamaduni na sanaa ya Kiislamu. Pallo Jordan amesema, nakala za maandishi ya mkono zinazoonyeshwa kwenye maonyesho hayo zinadhihirisha nafasi na mchango wa mafundisho ya dini ya Kiislamu katika kubainisha elimu, maarifa na mshikamano wa kitamaduni.
Ni vema kukumbusha hapa kuwa Waislamu ndiyo jamii ya pili kwa kuwa na wafuasi wengi nchini Afrika Kusini. 316186
captcha