Ofisi ya Mawasiliano ya Umma ya Kongamano la kimataifa la Filamu Fupi imetangaza kwamba kikao hicho kitahudhuriwa na wawakilishi wa nchi za Lebanon, Tajikistan, Tunisia, Pakistan, Sudan, Iran na Afghanistan.
Katika kiikao hicho wajumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Watengezaji Filamu Fupi kutoka nchi za Kiislamu watachunguza na kutathmini utendaji kazi wa mwaka mmoja uliopita wa jumuiya hiyo na kuweka mikakati ya mustakbali washughuli zake.
Kikao hicho kitafanyika sambamba na kongamano la Filamu Fupi litakaloanza mjini Tehran kuanzia tarehe 12 hadi 17 mwezi huu wa Novemba. 316800