Hayo yamesemwa na Khalil Noudehi msanii wa mwandishi na michoro ambaye kazi zake za kisanii zilionyeshwa katika mwezi wa Ramadhani uliopita huko Kuwait chini ya usimamizi wa Taasisi ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu ya Iran. Khalil Noudehi amesema kuwa harakati kama hizo za kitamaduni zina umuhimu na mchango mkubwa katika kuarifisha turathi za Kiislamu, kiqurani na sanaa na wasanii wa Kiislamu. Amesema kwamba ulimwengu wa Kiislamu una wasanii wengi wakubwa ambao kazi zao zimepuuzwa na baadhi yazo zinahifadhiwa katika majumba ya makumbusho ya kimataifa.
Noudehi amesisitiza juu ya udharura wa kukusanywa kazi na athari za wasanii hao na kuarifishwa kwa walimwengu. 316365