IQNA

Mkuu wa Unesco atembelea kituo cha habari na nyaraka za Kiislamu

15:22 - November 10, 2008
Habari ID: 1706730
Chonly Han, mwakilishi na mkuu wa ofisi ya kieneo ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa nchini Iran akiandamana na Ali Ashraf Mujtahid Shibstari, Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu nchini Iran, jana Jumapili walitembelea ofisi ya utafiti ya Tasisi ya Uhubiri wa Kiislamu ya Chuo cha Kidini cha Qum
Maafisa wawili hao walizungumza na kujadiiana na wakuu wa kituo hicho cha habari na vyaraka za Kiislamu kuhusu njia za kuimarisha ushirikiano wa pande mbili. Ni vyema kuashiria hapa kwamba, kituo kilichotajwa kimekusanya na kuandaa vitabu na nyaraka muhimu za Kiislamu zikiwemo Istilahi zinazotumika katika mafundisho na elimu za Kiislamu, jambo ambalo limewavutia maafisa wa Unesco. 317691
captcha