IQNA

Masuala ya kidini na kikabila yazusha utata Bulgaria

15:39 - November 10, 2008
Habari ID: 1706740
Kufunguliwa kwa chama kipya cha Kiislamu nchini Bulgaria kumezusha mjadala mkali wa kidini na kikabila nchini humo.
Suzgan Mumin mmoja wa wanasiasa mashuhuri wa Bulgaria wiki iliyopita alijitenga na chama cha Wabulgaria wenye asili ya Kituruki na kutangaza rasmi kubuni chama kipya cha kisiasa nchini humo. Ripoti kutoka nchini humo zinasema kuwa, suala la kwanza litakalojadiliwa na chama hicho ni kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa jamii ya Waislamu wa Kibumag nchini humo. Kutangazwa rasmi kuwepo kwa jamii hiyo nchini Bulgaria kumezusha hisia mbalimba. Hisia hizo hata zimempelekea Waziri Mkuu Sergei Stanishev na Rais Georgi Parvanov wa nchi hiyo kuandaa kikao cha kujadili jambo hilo. Rais Parvanov amesema kuwa, kuchochea hisia za kidini na kikabila nchini Bulgaria na sawa na kuchezea moto na kuzitaka pande husika kutumia mantiki na kutochafua jina zuri la nchi hiyo kutokana na kuishi kwa pamoja kwa amani wananchi wake ambao ni wafuasi wa dini na makabila mbalimbali. Viongozi na makundi mbalimbali ya Bulgaria yamekemea hali na mjadala huo mpya uliojitokeza nchini Bulgaria kuhusiana na suala la udini na ukabila na kumtaka Suzgan Mumin kuomba msamaha kwa kutumia neno Bumag. Hii ni katika hali ambayo Mumin anasisitiza kwamba, kabila hilo la wachache liko nchini humo na kwamba hakuna mtu yoyote anayeweza kupinga ukweli huo. 317687
captcha