Msemaji wa Baraza la Elimu la mji wa Vienna amesema, Bulat Amina, mmoja wa wanawake hao ambaye ana asili ya Uturuki, ameruhusiwa kufundisha katika mojawapo ya shule za msingi za mji huo. Amesema kuwa kuteuliwa mwalimu mwanamke mwenye asili ya Uturuki kutatoa mchango mkubwa katika shule za Vienna kwani idadi kubwa ya shule za mji wa Vienna zina wanafunzi wa Kiaustria wenye asili ya Uturuki.
Kuruhusiwa walimu wenye vazi la hijabu kufundisha katika shule za Austria hakujazusha matatizo wala malalamiko ya aina yoyote na hadi sasa hakuna sheria inayozuia vazi la hijabu wakati wa kufunza mashuleni nchini humo. Hii ni katika hali ambayo uvaaji wa vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu (hijabu) mashuleni umezusha matatizo katika nchi za Ufaransa na Ujerumani na hatimaye walimu wa kike wenye vazi hilo wamepigwa marufuku kufunza katika shule za nchi hizo. 317843-