IQNA

Haki ya kurejea Wapalestina katika ardhi yao yachunguzwa katika kikao cha kimataifa huko Syria

14:23 - November 11, 2008
Habari ID: 1707116
Kongamano la kimataifa la, "Haki ya Kurejea Wakimbizi Wapalestina Katika Ardhi yao" litafanyika tarehe 23 Novemba katika mji mkuu wa Syria, Damascus na kuhudhuriwa na shakhsia elfu nne wa ngazi za juu Waislamu na wasiokuwa Waislamu.
Shirika la habari la Xhinhua limemnukulu Abdul Aziz Said, Katibu Mkuu wa Kongamano la Kitaifa la Kutetea Quds akisema kuwa mipango ya mkutano huo wa kuunga mkono haki ya wahajiri wa Kipalestina kurejea katika ardhi yao ambayo mji mkuu wake utakuwa Quds, imekamilika.
Abdul Aziz Said ameongeza kuwa, lengo la kuandaliwa kongamano hilo ni kuunga mkono haki ya kurejea makwao wahajiri wa Kipalestina. Aidha washiriki wanatarajiwa kupinga maelewano ya PLO na utawala ghasibu wa Israel na kusisitiza kwamba, wakimbizi wa Kipalestina hawatakubali kubadilisha ardhi zao asili na eneo lolote lile.
Mwanaharakati huyo amebainisha kuwa mkutano huo wa kimataifa utasisitiza juu ya udharura wa kutekelezwa haki za Wapalestina kwa mujibu wa uadilifu na sheria za kimatiafa. Vile washiriki watalaani jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina ambazo zinafanyika katika fremu ya mauaji ya kimbari katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Taasisi 50 za Kipalestina, Kiarabu, Kiislamu na Kimataifa, zitashiriki katika kongamano hilo. 318295

captcha