IQNA

Utawala wa Israel umetenga dola bilioni tano kwa ajili ya kuuyahudisha mji wa Quds

10:34 - November 12, 2008
Habari ID: 1707375
Raif Najm, Waziri wa zamani wa Wakfu wa Jordan na mtaalamu wa masuala ya Quds na Msikiti Mtukufu wa al-Aqsa amesema kuwa utawala haramu wa Israel umetenga dola bilioni tano kwa ajili ya kuufanya mji mtakatifu wa Quds kuwa wa Kiyahudi.
Raif Najm alitoa taarifa hapo jana Jumatatu akisema kuwa, hatua za uharibifu za utawala wa Kizayuni ni hatari kubwa kwa utambulisho wa Kiislamu wa Msikiti wa al-Aqsa na utambulisho wa Kiislamu na kihistoria wa mji mtukufu wa Quds pamoja na urithi wa kiutu wa mji huo. Akizungumzia hatua za kiudui dhidi ya Uislamu na Waislamu zinazotekelezwa na utawala haramu wa Israel katika mji huo na hasa kuhusu Msikiti wa al-Aqsa, Raif Najm amesema kuwa hivi sasa askari wa utawala haramu wa Israel wanachimba njia za chini kwa chini katika nsikiti huo na kuziunganisha na vitongoji vya Mayahudi. Katika taarifa hiyo, Najm amezikosoa vikali nchi za Kiislamu na Kiarabu kwa kukaa kimya mbele ya hujuma hiyo kubwa ya Wazayuni ya kutaka kuufanya mji huo mtakatifu kuwa wa Kiyahudi na kuongeza kuwa iwapo nchi hizo zitaendelea kunyamaza bila shaka utawala huo ghasibu utaendelea kutekeleza mipango yake hiyo hatari katika mji huo wote katika miaka ijayo. Najm ameashiria kuwepo kwa zaidi ya mahekalu kumi ya Mayahudi katika mji wa Quds na kusema kuwa hekalu la mwisho lilifunguliwa na Wazayuni umbali wa mita 50 kutoka katika Msikiti wa al-Aqsa mwezi Oktoba uliopita. Amesema kuwa katika hali ya hivi sasa utawala haramu wa Israel unafikiria kujenga hekalu kubwa zaidi la Mayahudi ulimwenguni katika mji huo. 318795
captcha