Wataalamu kutoka nchi za Iran, Canada, Bangladesh, India, Jordan, Lebanon, Uingereza, Umoja wa Falme za Kiarabu na Pakistan wamewasilisha makala mbalimbali katika mkutano huo.
Lengo la mkutano huo unaosimamiwa na Kitivo cha Sanaa cha Chuo cha Lahore, Chuo Kikuu cha Punjab na jumba la makumbusho la mji wa Lahore ni kustawisha utafiti katika nyanja za sanaa na usanifu majengo wa Kiislamu. 318868