IQNA

Taasisi ya utafiti kuhusu uwekezaji wa Kiislamu yaanzishwa Malaysia

11:57 - November 13, 2008
Habari ID: 1707752
Taasisi ya utafiti kuhusu uwekezaji wa Kiislamu imeanzishwa siku ya Jumanne huko Kuala Lumpur, Malaysia katika sherehe zilizohudhuriwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdullah Ahmad Badawi.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Barnama, akihutubu katika hafla hiyo, Waziri Mkuu wa Malaysia ametoa mwito kwa wataalamu wa uchumi wa Kiislamu kuyaonyesha masoko ya dunia kuwa mfumo wa uwekezaji wa Kiislamu ni endelevu na wenye kuaminiwa.
Ameongeza kuwa: 'mgogoro wa hivi karibuni wa fedha duniani ni fursa ya kuthibitisha kuwa mfumo wa uwekezaji wa Kiislamu ni endelevu na kwa hivyo tunapaswa kutumia fursa hii kwa njia bora'.
'Sisi tunapaswa kuzidisha jitihada za kueneza uwekezaji wa Kiislamu na kuondoa vizingiti vilivyopo' amesema Badawi.
Waziri Mkuu wa Malaysia aidha amesema kuwa, kuanzishwa taasisi hii ni fursa muafaka ya kuandaa mazingira ya ushirikiano baina ya wasomi wa Kiislamu kutoka nchi mbali mbali kwa lengo la kustawisha uwekezaji wa Kiislamu na kuanzisha kanuni za uendeshwaji harakati za kifedha katika nchi za Kiislamu. 319555

captcha