Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO Abdulaziz Othman al Twaijri amemtangaza Jean Poul Cartron katika Baraza la Seneti la Ufaransa kuwa balozi wa ISESCO katika mazungumzo kati ya tamaduni mbalimbali.
Mwandishi wa IQNA ameripoti kuwa uamuzi wa kuteuliwa Jean Poul Cartron kuwa mwakilishi wa ISESCO ulichukuliwa katika kikao cha 29 cha Baraza la Utekelezaji la shirika hilo kilichofanyika mwezi Juni mwaka huu nchini Morocco.
Baadhi ya shakhsia wa kielimu, kiutamaduni, viongozi wa serikali ya Ufaransa na wanadiplomasia wa nchi za kigeni walihudhuria kikao cha kumuarifisha mwakilishi wa ISESCO. 319525